tatanyengo
JF-Expert Member
- Mar 30, 2011
- 1,133
- 280
Ni takribani miezi mitano impepita sasa tangu mahafali ya kwanza ya Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) ifanyike na kuhudhuriwa pia na mkuu wa nchi ambaye alitunukiwa shahada ya uzamivu. Jambo la ajabu na la kusikitisha ni kwamba hadi sasa wahitimu hao hawajapewa Transcripts zao. Hali hii imeawasababishia usumbufu mkubwa kwani wanashidwa kuomba kazi au kupandishwa vyeo/madaraja makazini kwao.Wanapofuatilia wanapewa majibu rahisi tu njoo baada ya wiki moja, njoo baada ya wiki mbili au mwezi. Tunaomba mamlaka husika zisaidie ili wahitimu hao wapate haki yao.