Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Zipo seti kuu mbili za dhima za Vyombo vya Habari nyakati za uchaguzi, ya kwanza inatokana na msimamo wa Kitaaluma ikiunganishwa na Wajibu wao kwa jamii, ya pili ni wajibu wa Kisheria wa Vyombo vya Habari.
Andiko la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kuhusu Vyombo vya Habari na Uchaguzi Mkuu 2020 linaeleza Vyombo vya Habari hutekeleza wajibu wake kwa kuarifu, kuelimisha, na hatimaye kuwajengea uwezo Wananchi kwa kuwapatia taarifa sahihi, zinazotoka kwa wakati, zilizowekwa kwenye muktadha, zilizofanyanyiwa utafiti na zinazohusiana na mchakato mzima wa Uchaguzi.
Hii inajumuisha kuwaleta pamoja raia ili kuchukua hatua na kushiriki kwenye chaguzi. Hivyo, Vyombo vya Habari ni kitu muhimu na kisichoepukika ili kuwa na Uchaguzi huru na wa Haki.