Hili suala lipo serious sana.Kwa ujumla eneo la Nyasura lina idadi kubwa sana ya wahalifu.Awali walijikita katika kuiba na kupora mali za raia ila kwa sasa hali imekuwa tofauti kabisa.
Kundi hili la wahalifu na vibaka wameanza kuvizia na kushambulia wanafunzi.Kila walipo hutembea na visu na aina nyingine za silaha hatarishi.
Matukio haya yameanza lini?
Wiki Jana kijana mmoja alijipenyeza eneo la shule kwa kupitia njia za vichochoroni ambapo lengo lake lilikuwa kumtafuta mwanafunzi mmoja ili amchome kisu. Japo lengo halikufanikiwa mhalifu huyu alimjeruhi kwa kisu mmoja wa walimu katika shule husika.
Tukio la pili
Jana siku ya ijumaa ilikuwa ni siku ya michezo(UMISETA SUB-CLASTER)Michezo hii ilihusisha shule nne ambazo ni Dr. Nchimbi, Kabasa, ACT Bunda girls, Mkwezi na Wariku. Kundi la wahalifu likiwa na silaha na lilifanikiwa kupora wanafunzi vitu vya thamani mfano pesa nk. Kama hilo halitoshi baada ya wanafunzi kutawanyika kundi hili lilianza kufuatilia baadhi ya wanafunzi ili kwenda kuwadhuru. Haijulikani kilichojiri maana ilikuwa jioni sana!Bado hatujapata kilichojiri.
Kwa nini kundi hili la vibaka lianze kushambulia wanafunzi?Kuna agenda gani?
Mpaka Sasa haijajulikana wazi sababu ya wahalifu hawa kuvizia wanafunzi na kuwashambulia.Vyombo ya ulinzi na usalama wafanye kila jitihada kuwalinda watoto wa shule.Ni wajibu wao na siyo ombi!
Na wakishindwa tutalifikisha kwa waziri wa mambo ya ndani na hata mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano kwa hatua zaidi.Basi kama inahitajika msaada wa JWTZ tujue.
Madhara ya uzembe wa kutolishughulikia hili kundi:
1.Itaweza kuongezea hofu kubwa sana kwa wanafunzi na kuwaathiri kisaikolojia.
2.Maafa makubwa yanaweza kutokea
3.
Maoni yangu binafsi(Nionavyo Mimi)
Sijaona kama kuna mikakati madhubuti ya kuwakabili hawa wahalifu sijajua tatizo lipo wapi uoga, kujuana, uzembe kwa wahusika au suala husika halina maslahi binafsi kwa wanaotakiwa kudhibiti uhalifu huu. Hili ni fumbo la Imani! Jamaa wanajiamini kweli yaani mchana mchana tena bila kufunika nyuso zao na bado wanadunda tu mtaani!
Usipoziba ufa utajenga ukuta, hatuombei mabaya yatokee ila wahalifu hawa wakifanikiwa kutimiza malengo yao ya uhalifu eneo hili itakuwa ndio mwanzo wa kudhuru wanafunzi wa shule nyingine pia.
Time will tell😭
Kwaresma njema na Mfungo mwema wa Ramadan!