DOKEZO Vyombo vya Usalama Mkoani Kagera au Taifa mchunguzeni Alistides Ndibalema na familia yake wa Kijiji cha Buzi Bugabo Bukoba

DOKEZO Vyombo vya Usalama Mkoani Kagera au Taifa mchunguzeni Alistides Ndibalema na familia yake wa Kijiji cha Buzi Bugabo Bukoba

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

mimi_wewe_sisi_wale

New Member
Joined
Jan 14, 2025
Posts
1
Reaction score
2
Wadau katika zunguka yangu katika Mkoa wa Kagera leo nimefika katika kijiji kimoja kinaitwa Buzi tarafa ya bugabo huko Bukoba vijijini. Hiki kijiji niliwahi kusoma taarifa zake hapa na masuala ya uchawi, n.k na kuna mdau aliandika mengi kwamba yanayosemwa ni masuala ya kusadikika.

Lengo la kufika huku ilikuwa ni kuona fursa hasa kwenye masuala ya ardhi baada ya kusikia tarafa hii na vijiji vyake ni moja ya sehemu ambayo manispaa ya bukoba ina mpango wa kuyachukua na kupanua eneo lake na kwamba kijiji hiki kina eneo zuri liliotengwa na serikali ya kijiji kwa shughuli za kilimo na ufugaji na lina maji. Mimi ni mdau wa kilimo cha mpunga.

Ni kijiji kikubwa na nimeambiwa wapo kwenye taratibu za kuona namna ya kuwa Kata. Kutoka town hadi wanaposema ni center ya kijiji ni kilometa 26.

Nimekuta tayari wameanza kujenga shule ya Sekondari na kwamba miaka ya 90 walishapata wadau kutoka kwenye hicho kijiji waliojenga msingi wa majengo ya sekondari na wanafunzi walianza kusoma kwa kutumia madarasa ya shule ya msingi Kashanje lakini hapo kati wadau walikosa nguvu na wengi walishatangulia mbele ya haki.

Kwasasa wadau kutoka kijijini hapo wanaoishi nje ya kijiji na mkoa wakishirikiana na wanakijiji wanaoishi huko wameanza tena ujenzi wa shule mpya katika eneo tofauti na la kwanza na wamekwisha jenga madarasa 3, vyoo na maabara 3 ambazo zipo hatua ya ukamilishaji. Hapa wanahitaji pia kutiwa nguvu na moyo.

Kilichonifanya niandike hapa ni kwamba walilazimika kujenga shule katika eneo inapojengwa kwasasa ili kutosimamishwa na mgogoro wa ardhi ulioanzishwa na familia ya bwana Alistides Ndibalema maarufu Kasaija (nimeambiwa maana yake ni kamwanaume) kwenye eneo ambalo tayari serikalli ya kijiji walishalitenga na kujenga Zahanati mpya tofauti na waliyokuwa nayo zamani, kumega eneo kwa ajili ya vyama vya siasa, eneo la ofisi za kata na kubainisha eneo litakalojengwa Shule ya Sekondari na maeneo mengine yaliyotengwa tayari kwa watu wanaotambulika na jamii nzima ya kijiji na yanatumika kwa ajili ya kulisha mifugo na mengine kwa ajili ya kulima huku yakisubiri matumizi rasmi yaliyobainishwa na serikali ya Kijiji.

Nimeambiwa familia hii kwasasa imetengwa na wanakijiji na wanaoingia kwao ni wale majirani waliopakana nao tu na wanakijiji hawashirikiani nao kwa chochote sababu kuu hasa ikiwa ni kuvamia eneo hilo na kujimilikisha wakati hawana umiliki wowote.

Kilichoniuma ni kuambiwa suala la familia hii kuleta watu kutoka Rwanda na Burundi na kuwatumia katika zoezi zima la kufanya mashambulizi kwa wananchi ikiwa ni pamoja na kuwakata mapanga wanaojitokeza kuongelea hilo eneo kwa kuwa wanalifahamu fika.
Nimeambiwa wapo watu wamekatwa vidole na hao watu kutoka Rwanda na Burundi wanaoletwa na hiyo familia.

Nimeambiwa mgogoro huu ushafikishwa mpaka ngazi ya Wilaya lakini hakuna utatuzi wowote badala yake wale wanaotokea kupaza sauti zao wanawekwa ndani bila kujua historia ya eneo. Kwamba Serikali ya kijiji iliyochaguliwa mwaka 2024 tayari baadhi wameshatishiwa wasiongelee hilo suala.

Nimeambiwa wanachi mpaka vijana wa makamo wanafahamu hilo eneo kwa undani na mpaka lilivyokuwa linatumika na wakulima wadogo wadogo wa chai kwamba wazee walihakikisha wanawaeleza kizazi na kizazi hilo eneo ni la kijiji na si mtu binafsi.

Vyombo vya ulinzi mchunguzeni huyo mtu kwa maana nimeumia kuambiwa wananchi wanaotetea eneo kwa ajili ya maendeleo ya kijiji wanakatwa mapanga na wanyarwanda na burundi wanaoletwa na hiyo familia.

Kwa urahisi wa kuijua familia hii ni huyo jamaa aliwahi kugombea ubunge bukoba mwaka 2015 kupitia CHADEMA (hapa wananchi nimeambiwa mgogoro hauna chembe yoyote ya siasa). Fikeni katika hicho kijiji mfanye kazi yenu kwa sababu nimeambiwa pia wapo mabinti wengi sana wanaoingia na kutoka kwenye hicho kijiji wakitokea Karagwe lakini wanasema kwa ufupi ni wa kulee.

Nimeoneshwa tangazo la mkutano wa kijiji utakaofanyika tarehe 16/01/2025 wakiwa na ajenda ya maendeleonya ujenzi wa sekondari Buzi na masuala ya mapato na matumizi. Tumieni mkutano huo kuwasiliza hao wananchi sababu inaonekana uongozi wa kijiji tayari umekwama, wilaya pia, sijajua upande wa mkoa.
 
Hilo kabila lenye wssomi wabobezi ila wanafanya vitu vya hovyo.

Waliwahi kuchoma shamba la Bishanga miaka hiyo.
 
Back
Top Bottom