Vyombo vya Usalama visifanye kazi kama Makundi ya Kijambazi

Bams

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2010
Posts
19,362
Reaction score
48,879
Tanzania ipo katika giza nene la kiutawala. Tatizo kubwa ni Serikali na watawala.

Watanzania tunalalamikia katiba mbaya, lakini ukweli ulio wazi, hata hiyo katiba yenye kasoro nyingi, haifuatwi wala kuheshimiwa na watawala na vyombo vya dola.

Katiba na sheria zetu zinaeleza na kutoa muongozo wa kila chombo cha Serikali kinavyotakiwa kufanya kazi. Lakini kwa bahati mbaya sana, kwa muda mrefu sasa, vyombo vya usalama, mara nyingi vimekuwa vikifanya kazi kama makundi ya kijambazi.

Wakati wa utawala wa Kikwete, tulishuhudia wakati wa mgomo wa madajtari, kiongozi wa madaktari, Dr. Ulimboka akitekwa na wanaohisiwa kwa asilimia kubwa kuwa maafisa usalama kwa njia za kijambazi, na kisha kumtupa msituni baada ya kumtesa na kumjeruhi.

Wakati wa utawala wa Hayati, matukio hayo yakaongezeka, na watenda ushetani huo na wasimamuzi wao, wakapewa nguvu kubwa ndani ya Serikali, na baadhi yao tunaowajua bado wapo ndani ya Serikali. Idadi ya watu waliotendewa uharamia huo ni kubwa, na baadhi ya wahanga wa matukio hayo mpaka leo hawajapatikana.

Na katika utawala huu wa Samia, mambo haya ya kihayawani, japo yamepungua, inaonekana bado yanaendelea. Sote tumesikia jinsi alivyotendewa mkosoaji wa Serikali, kijana Edgar. Siamini kama ni maagizo ya moja kwa moja ya Rais, lakini uwepo wa haya majitu yenye tabia hizo za kishetani ndani ya Serikali, za kuteka watu, kunayafanya matukio haya kuendelea kuwepo.

Kama kuna mtu ametenda makosa au uovu wowote, taratibu za kumkamata mtuhumiwa zipo wazi kisheria. Polisi au TISS hawatakiwi kufanya kazi kama magenge ya majambazi. Mtuhumiwa anatakiwa kukamatwa kwa uwazi, na polisi wanatakiwa kujitambulisha. TISS nao wana taratibu zao, na hawana mamlaka ya kuwateka watu kama majambazi.

Huu uharamia unaofanywa na watendaji hayawani ndani ya vyombo vya ulinzi na usalama, unaendelea kwa sababu watawala ama wameubariki au kwa sababu hawaumizwi wala kukerwa nao. Kama wasingekuwa wanautaka, hakika ungekoma. Watawala wetu, kwenye vinywa vyao wana maneno mazuri ya kuonesha wanajali uhai na haki za raia lakini bila shaka kwenye mioyo yao hawana chembe yoyote ya kupenda haki wala kuujali au kuuthamini uhai wa binadamu wenzao.

Hakika, anayewatesa, anaye anayewaua na anayewateka watanzania ni shetani, ni hayawani, ni adui wa kila Mtanzania. Tuukatae ushetani huu kwa njia zote zinawezekana. Tupaze sauti kwenye majukwaa yetu ya ndani mpaka kwenye majukwaa ya kimataifa, kuelezea ushetani unaoendelea Tanzania. Matukio haya ya sasa ni ishara tosha kuwa kuna uwezekano mkubwa, yakaongezeka sana kadri tunavyosogea kuelekea kwenye uchaguzi.

Hima Watanzania, tupiganie haki zetu, tupiganie uhai wetu. Vyombo vya ulinzi na usalama vifanye kazi kwa kufuata taratibu. Na kama vinataka kumkamata mtuhumiwa yeyote vifuate taratibu na vimkamate vikiwa kwenye sare rasmi. Tofauti na hapo, anayefanya kinyume, achukuliwe ni jambazi anayetaka kuudhuru uhai wa mtanzania mwenzetu. Kwa njia zozote zile ni halali katika kupambana na jambazi hilo.

Sote tunafahamu kuwa utekaji wote wa watu wanaoikosoa Serikali unafanywa na vyombo vya dola vikitenda kazi kama majambazi. Huu ushetani tusiukubali kamwe.
 
Uongozi wa hovyo watu wanaenda kinyume na viapo vyao vya kuwalinda watanzania
 
Dola imeruhusu wanausalama wa taifa kuwa chawa wa viongozi badala ya kuipambania jamuhuri!!

Eric uvccm wanakua wanausalama wa taifa!!!

Ni Tatizo kubwa sana!!

Watanzania wana haki zaidi kuandamana dhidi ya Serikali, kuliko hata Kenya.

Huu ushenzi wa kuteka watu wanaowakosoa watawala au Serikali, na wakati mwingine kuwaua, hautaisha, tukiendelea kuichekea CCM.
 
Lazima hao watekaji watakuwa wamesomea kwa Wazungu.

Labda Si yai Yei, Emu Fiteen, KGB, Kuba.

Ni kwamba, mnatuambia Watanzania tujivunze kutoka kwa Wazungu n.k, weshajivunza wanafanya, sasa mnasema huu ni Ushetani.

Kazi kweli.
 
Tanzania ipo katika giza nene la kiutawala. Tatizo kubwa ni Serikali na watawala.

Watanzania tunalalamikia katiba mbaya, lakini ukweli ulio wazi, hata hiyo katiba yenye kasoro nyingi, haifuatwi wala kuheshimiwa na watawala na vyombo vya dola.

Katiba na sheria zetu zinaeleza na kutoa muongozo wa kila chombo cha Serikali kinavyotakiwa kufanya kazi. Lakini kwa bahati mbaya sana, kwa muda mrefu sasa, vyombo vya usalama, mara nyingi vimekuwa vikifanya kazi kama makundi ya kijambazi.

Wakati wa utawala wa Kikwete, tulishuhudia wakati wa mgomo wa madajtari, kiongozi wa madaktari, Dr. Ulimboka akitekwa na wanaohisiwa kwa asilimia kubwa kuwa maafisa usalama kwa njia za kijambazi, na kisha kumtupa msituni baada ya kumtesa na kumjeruhi.

Wakati wa utawala wa Hayati, matukio hayo yakaongezeka, na watenda ushetani huo na wasimamuzi wao, wakapewa nguvu kubwa ndani ya Serikali, na baadhi yao tunaowajua bado wapo ndani ya Serikali. Idadi ya watu waliotendewa uharamia huo ni kubwa, na baadhi ya wahanga wa matukio hayo mpaka leo hawajapatikana.

Na katika utawala huu wa Samia, mambo haya ya kihayawani, japo yamepungua, inaonekana bado yanaendelea. Sote tumesikia jinsi alivyotendewa mkosoaji wa Serikali, kijana Edgar. Siamini kama ni maagizo ya moja kwa moja ya Rais, lakini uwepo wa haya majitu yenye tabia hizo za kishetani ndani ya Serikali, za kuteka watu, kunayafanya matukio haya kuendelea kuwepo.

Kama kuna mtu ametenda makosa au uovu wowote, taratibu za kumkamata mtuhumiwa zipo wazi kisheria. Polisi au TISS hawatakiwi kufanya kazi kama magenge ya majambazi. Mtuhumiwa anatakiwa kukamatwa kwa uwazi, na polisi wanatakiwa kujitambulisha. TISS nao wana taratibu zao, na hawana mamlaka ya kuwateka watu kama majambazi.

Huu uharamia unaofanywa na watendaji hayawani ndani ya vyombo vya ulinzi na usalama, unaendelea kwa sababu watawala ama wameubariki au kwa sababu hawaumizwi wala kukerwa nao. Kama wasingekuwa wanautaka, hakika ungekoma. Watawala wetu, kwenye vinywa vyao wana maneno mazuri ya kuonesha wanajali uhai na haki za raia lakini bila shaka kwenye mioyo yao hawana chembe yoyote ya kupenda haki wala kuujali au kuuthamini uhai wa binadamu wenzao.

Hakika, anayewatesa, anaye anayewaua na anayewateka watanzania ni shetani, ni hayawani, ni adui wa kila Mtanzania. Tuukatae ushetani huu kwa njia zote zinawezekana. Tupaze sauti kwenye majukwaa yetu ya ndani mpaka kwenye majukwaa ya kimataifa, kuelezea ushetani unaoendelea Tanzania. Matukio haya ya sasa ni ishara tosha kuwa kuna uwezekano mkubwa, yakaongezeka sana kadri tunavyosogea kuelekea kwenye uchaguzi.

Hima Watanzania, tupiganie haki zetu, tupiganie uhai wetu. Vyombo vya ulinzi na usalama vifanye kazi kwa kufuata taratibu. Na kama vinataka kumkamata mtuhumiwa yeyote vifuate taratibu na vimkamate vikiwa kwenye sare rasmi. Tofauti na hapo, anayefanya kinyume, achukuliwe ni jambazi anayetaka kuudhuru uhai wa mtanzania mwenzetu. Kwa njia zozote zile ni halali katika kupambana na jambazi hilo.

Sote tunafahamu kuwa utekaji wote wa watu wanaoikosoa Serikali unafanywa na vyombo vya dola vikitenda kazi kama majambazi. Huu ushetani tusiukubali kamwe.
Mkuu ongezea hashtags hapo;
#KataaMachawa
#KataaWatuWasiyojulikana
#KataaUozo2025
 
Back
Top Bottom