Mag3
Platinum Member
- May 31, 2008
- 13,413
- 23,592
Haya ni maoni ya msemaji wa jeshi letu la ulinzi, JWTZ;
Wanajeshi wanapomaliza mafunzo yao kitu cha kwanza wanachokabidhiwa ni rungu kwa ajili ya kutimiza wajibu ikiwamo kudhibiti vurugu, huku akisisitiza kauli ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda juu ya kuwapiga watu wanaokaidi amri ya serikali.
Alipoulizwa kama viongozi hao wa CUF walikaidi amri na kuanzisha vurugu zilizowalazimisha JWTZ kuwapiga, Mgawe alimtaka mwandishi wa habari hizi awe mzalendo kwa taifa.

Ibrahim Lipumba said:Jumatatu, Julai 01, 2013 09:41- Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika kambi ya Naliendele, wamewafanyia mateso makubwa viongozi wa CUF, akiwemo Mkurugenzi wa Oganaizesheni, Uchaguzi na Bunge, Shaweji Mketo, ambaye alipigwa mpaka akazimia.
Kanali Kapambala Mgawe said:Sisi hatufanyi kazi kisiasa, sina uhakika kama askari wetu wanafanya mambo hayo, naelewa wapo Mtwara kulinda amani.
Advera Senzo said:Mwandishi Mwangosi alikuwa akikimbia kutoka upande wananchi na kuelekea walipokuwa Polisi akapigwa na kitu kilichorushwa kikitokea upande wa Wananchi (Chadema) na kumfikia ambacho kilimjeruhi pia Askari akiwamo Mkuu wa kituo cha Polisi.
Balaa yote hii ili mradi CCM ibaki madarakani! Picha zitafuatia...Msemaji wa JWTZ said:Suala la mwanamke kubakwa linaweza kutokea lakini si kwa kufanywa na askari wa wetu. JWTZ imefundishwa kuwa na nidhamu ya kazi, hali inayowafanya watu wasio waadilifu kutengeneza mazingira ya kulichafua kwa manufaa yao. Hata kama suala hilo lipo basi lisihusishwe na jeshi na badala yake ahusishwe mtu aliyefanya huo ukatili.