Vyombo vyetu vya ulinzi vimetugeuka, tukimbilie wapi wananchi wenzangu Watanzania?

Mag3

Platinum Member
Joined
May 31, 2008
Posts
13,413
Reaction score
23,592
Haya ni maoni ya msemaji wa jeshi letu la ulinzi, JWTZ;

Wanajeshi wanapomaliza mafunzo yao kitu cha kwanza wanachokabidhiwa ni rungu kwa ajili ya kutimiza wajibu ikiwamo kudhibiti vurugu, huku akisisitiza kauli ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda juu ya kuwapiga watu wanaokaidi amri ya serikali.

Alipoulizwa kama viongozi hao wa CUF walikaidi amri na kuanzisha vurugu zilizowalazimisha JWTZ kuwapiga, Mgawe alimtaka mwandishi wa habari hizi awe mzalendo kwa taifa.


Ibrahim Lipumba said:
Jumatatu, Julai 01, 2013 09:41- Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika kambi ya Naliendele, wamewafanyia mateso makubwa viongozi wa CUF, akiwemo Mkurugenzi wa Oganaizesheni, Uchaguzi na Bunge, Shaweji Mketo, ambaye alipigwa mpaka akazimia.
Kanali Kapambala Mgawe said:
Sisi hatufanyi kazi kisiasa, sina uhakika kama askari wetu wanafanya mambo hayo, naelewa wapo Mtwara kulinda amani.
Advera Senzo said:
Mwandishi Mwangosi alikuwa akikimbia kutoka upande wananchi na kuelekea walipokuwa Polisi akapigwa na kitu kilichorushwa kikitokea upande wa Wananchi (Chadema) na kumfikia ambacho kilimjeruhi pia Askari akiwamo Mkuu wa kituo cha Polisi.
Balaa yote hii ili mradi CCM ibaki madarakani! Picha zitafuatia...
 


Wasemaji wa vyombo vyetu vya JWTZ na Polisi, kwa kukanusha ukweli hawajambo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…