DOKEZO Vyoo vya Hospitali ya Vijibweni Kigamboni ni vichafu na vimechoka kuliko maelezo

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Hospitali ya Vijibweni Kigamboni ndani ya Dar es Salaam kuna kero ya vyoo ambayo ni hatari kwa watumiaji.

Your browser is not able to display this video.

Your browser is not able to display this video.

Vyoo hivyo vya ni vichafu kwa ndani, vinanuka harufu kali mno kuna uchakavu mwingi pia sasa ni zaidi ya miezi mitatu hakuna taa za chooni na chache zilizopo haziwaki, kila nikienda hapo nakutana na hali hiyo.

Video na picha hizi nimezirekodi usiku nilipoenda kuchukua majibu ya vipimo, hizi zipo upande wa Vyoo vya Wanaume ila nimejulisha kuwa Upande wa Wanawake vyoo vyao hali ni mbaya zaidi.

Hapo inapoanza kuonesha giza nilianza kwa kuwasha switch ya taa zaidi ya mara nne haikufanya kazi, ndipo nikawasha mwanga was imu yangu na kumulika muonekano wa choo na sinki la kunawia mikono pia na ndoo ya chooni ambayo yenyewe wakati wote hainaga maji hali inayosababisha watu kujisaidia bila kumwaga maji wala kujisafisha.
===
Pia soma Mbunge wa Kigamboni aahidi kulifanyia kazi suala la uchafu na uchakavu wa vyoo vya Hospitali ya Vijibweni
 
Mkuu pole sana ila pale sio sehemu ya kupeleka mgonjwa ji majanga matupu.
 
Subiri rais Samia kasafiri na timu ya chawa 700 nje ya nchi, wakirudi watavitengeza.
 
Manispaa ya Kigamboni sijui wanafanya nini?
Barabara mbovu
Hospital mbovu
wananchi wanajitahidi kuwekeza ila serikali sasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…