Vyovyote vile, kwa faida ya afya ya mwili na akili, zoezi zuri la kawaida ni lile linaloshughulisha mwili mzima

Joined
Oct 5, 2015
Posts
90
Reaction score
482
Mazoezi burudani.
Ukiachana na mazoezi makali ya kijeshi ambayo hufanywa kwa malengo maalum, mtu anaweza kuuweka mwili wake kwenye afya imara kwa kufanya mazoezi huku akiburudika.
Ingawa wengine huamua kwenda 'Gymn' kutengeneza kifua, mkono (tricepts, bicepts) mabega, tumbo, shingo, boobs &, butts (kwa wanawake) nk, baadhi huamua kujifanyisha mazoezi yao wenyewe; kukimbia, kupiga pushup, kuruka kichura nk.
Vyovyote vile, kwa faida ya afya ya mwili na akili, zoezi zuri la kawaida ni lile linaloshughulisha mwili mzima - na kutoka jasho jingi.

Watu wengi hukosa muda au hupata uvivu wa kufanya mazoezi, au kwa sababu ya u-bize wa biashara, kazi na ajira, masomo na mengineyo. Hawajui, mazoezi ya mwili yangewasaidia sana kwenye hayo mambo yanayowaweka 'bize'.

"Mapigo ya moyo yataimarika na kusukuma damu kwa kasi inayohitajika ili kusambaza virutubisho, hewa ya oxygen, vitamini, homoni na enzymes - kuelekea sehemu zote za mwili vinapohitajika. Figo itachuja damu vizuri na kuondoa sumu zilizozalishwa kwenye misuli na ogani zingine za mwili, mapafu yataingiza hewa safi ya oxygen kwa wingi, na kuruhusu hewa - sumu ya 'carbodioxide' itoke haraka, ngozi itachuja chumvichumvi za ammonia na takataka nyingine za mwili".
Akili itakaa sawa, kumbukumbu zitadumu, mwili utajengeka kwa siha na haiba. 'Stress' zitapungua, ngozi itakuwa angavu' na kinga ya mwili itaimarika. Zaidi, maradhi ya akili na mwili yatasogea mbali nawe.

Lakini muda wa mazoezi hakuna!

Usiwaze Sana. Unaweza kucheza muziki? Unaweza kuogelea? Unapenda kufanya 'sex'?

Hayo ni mazoezi hasa, na faida yake kiafya ni ileile inayopatikana kwenye mazoezi mengine, ukiacha mazoezi ya kijeshi na yale ya kujenga viungo vya mwili.
Jifungie chumbani - fungulia muziki unaopenda - cheza mikono na miguu - utoke jasho ukaoge - hata mara tatu kwa wiki inatosha? Utakosa muda wa kufanya hivyo?

Sex? Fanya sex na umpendaye, shughulisha viungo vyote vya mwiki jinsi unavyoweza - toka jasho jingi ukaoge. Utashindwa kufanya hivyo mara moja kwa wiki?

Kuogelea? Hii ni kwa wanaoweza kuogelea. Kuogelea ni mazoezi matamu sana yanayotumia nguvu kubwa lakini unaburudika. Kwa bahati mbaya mazingira yetu ya kitanzania hayana maeneo mengi ya kuogelea - bahati yake anayeweza kupata fursa hiyo...ni mazoezi ya 'raha' sana.

Basi! Hayo ndio mazoezi - burudani; Unajenga mwiki huku unapata raha - kwa wale wasiopenda kujitesa na vyuma vizito au kukimbia na magari barabarani..

Usisahu kunywa maji ya kutosha; mengi unavyoweza.
Asante.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…