Vyuku vya Marrybrown,vinakaangwaje

Vyuku vya Marrybrown,vinakaangwaje

mfianchi

Platinum Member
Joined
Jul 1, 2009
Posts
11,904
Reaction score
8,371
Jamani nimekuwa mtumwa wa vyuku(kuku) vya kwenye mgahawa wa Marrybown,kwa anyejua jinsi vinavyotayarishwa kwani nataka niwe najitengenezea mwenyewe badala ya kutoa book 11 na nusu kila nikivimind
 
kuna chef mmoja yuko Marry Brown M City nitamuuliza kama ana maujuzi

then nitakwambia
 
huwa wanachanganya na unga wa ngano wenye mayai..
 
Watakuwa ndo wanapikwa hivi, unawaweka viungo wakiwa wabichi vile. Unapiga yai kwenye bakuli, unachovya kipande kwenye mayai kiloe then unakigeuza geuza kwenye unga wa ngano ulioutawanya kwenye sahani pana au sinia kinanata unga vizuri na kwa cheupe ndipo unakaanga kwenye mafuta kama andazi vile knaiva na kuwa na brownish.
 
kama ndio hivi basi najua. ila kama unatumia kuku wa kienyeji inabidi uwachemshe kwanza ndipo uwakaange. Mie kuku wa kizungu shida sana kuwala.
 
Sijawahi kula hao wa MB lakini najua kwamba wa kukaanga kwa style hiyo unaweza ukaweka bread crumbs(chenga chenga za mkate) badala ya unga wa ngano. Inaongeza ladha zaidi.
 
kama ndio hivi basi najua. ila kama unatumia kuku wa kienyeji inabidi uwachemshe kwanza ndipo uwakaange. Mie kuku wa kizungu shida sana kuwala.
style hii inatumika sana kwa kuku wa kizungu kwa sababu walaini, kitu kingine ni kwamba kwasababu huwa hawana utamu kivile kama wa kienyeji ndo mana wakabuniwa mapishi.ya hivi kuboresha ladha.
 
ni kweli lakini hao kuku wa kukua wiki mbili aaah! taabu kwelikweli.
 
Jamani nimekuwa mtumwa wa vyuku(kuku) vya kwenye mgahawa wa Marrybown,kwa anyejua jinsi vinavyotayarishwa kwani nataka niwe najitengenezea mwenyewe badala ya kutoa book 11 na nusu kila nikivimind

mdau wangu.. With a good heart... Wale kuku in a long run..yaani si wa kukubali kuzoeleka... Wana kasumu fulani hizi i cant recall well.. Kuna siku tulikuwa tuna discuss kwa mgonjwa fulani hivi.. Pia unene amabo hupelekea shinikizo la damu na kisukari ndugu yangu
 
Back
Top Bottom