Vyuo toeni selection msisubiri TCU

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Natoa wito kwa vyuo vingine kutoa selection zao na si kusubiri hawa TCU.Kuna watu wanasubiri hizo selection ili kama wamekosa wajiandae kwenda vyuo hata vya Diploma.Kuna vyuo kama hiki chuo kimoja watu wanatakiwa kuripoti kuanzia trh 20/08/2012 kwahiyo mtu unashindwa hata kujipanga vizuri kwani wengine wanatakiwa kuomba ruhusa makazini.Sasa leo uombe kwenda hicho chuo na kesho tena uombe kubadilisha kuwa umepata chuo kikuu.Huo sio usumbufu kwa mabosi?

Hata hiyo inayatuonyesha tuko admitted tuna wasiwasi nazo kwasababu hii system yenu haimaniki.Inawaza kukuonyesha uko admitted kumbe ukweli ni kinyume chake.

Ushauri mwingine process ya kuomba vyuo kupitia TCU ianze mapema na ikibidi hata january ili mpate muda wa kutosha kupitia maombi na kutoa selection mapema iwezekanavyo.
 
Wazo zuri sana!! ila hapo kwenye kuanza kwa uombaji iwe January Duuuu!! wakati tokeo linatoka mei
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…