Vyuo vikuu mtambueni shaaban robert

MAKOLE

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2012
Posts
618
Reaction score
280
Nashindwa kuelewa sababu ya huyu Shaaban Robert ambaye anafananishwa na shakespere hapa Tanzania kutopewa hata shahada ya heshima ili kuienzi kazi yake lakini kuna watu wanatunukiwa tu hizo shahada pasi na kustahili.
 
Nashindwa kuelewa sababu ya huyu Shaaban Robert ambaye anafananishwa na shakespere hapa Tanzania kutopewa hata shahada ya heshima ili kuienzi kazi yake lakini kuna watu wanatunukiwa tu hizo shahada pasi na kustahili.
Mfano huyu mruka nje kila uchao eti alitunukiwa Shahada ya Heshima ya Uzamivu kaatika Sheria (kwa kusuluhisha migogoro katika afrika) ya UDSM last year wakati mikataba mibovu na ya kihuni inafanyika chini ya uongozi wake kila uchao toka akiwa waziri wa nishati, nje na sasa ndo bwerereeeeeeeeeeeeeeeeeeee. Je, huyu anaweza hata kufunga viatu vya Shaban Robert?? Siasa zikingia kwenye elimu nchi haina tija tena na hatimaye ni taifa mfu lisilo na fikra pevu na komavu katika kujiletea maendeleo. SHABAN ROBERT atakuja tambuliwa na viongozi na wanazuoni wasiokuwa na mlengo wa siasa na elimu za kutibu njaa!!!!
 
Shaban Robert ni mtunzi mahiri mno wa wakati wake na wakati huu. Anastahili tuzo nyingi. Yupo daraja la kina Kezilahabi, Ibrahim Hussein n.k. Falsafa aliyoweka kitabu cha ''Kufikirika" na "Kusadikika" ni nzito na ni kama zinaicheka Tanzania ya leo ktk uongozi mbaya, ufisadi, umbumbumbu ktk mikataba n.k. Tutamuenzi sie wanyonge wenzake.
 

Kezilahabina IbrahimHussein hawawezi kuwa daraja moja na Sheikh Shaaban Robert. Kumbuka kuwa sheikh aliishia darasa la nne la mkoloni. Huyo Robert alikuwa na kipaji ktk lugha ya kiswahili si kwakusoma kwake, bali kuzaliwa. Huu ni mtazamo wangu baada ya kusoma kozi ya fasihi linanishi.( comperative literature)
 

Kuna mwingine watu wengi hawamkumbuki lakini alitoa mchango mkubwa sana katika kukuza lugha ya kiswahili si mwingine bali Mathias Mnyampala!!
 
mkuu hii nchi ni ya kusadikika na watu wake kama unavyowaona ni wakusadikika na heshima ya Shaaban Robert ni yakusadikika. Shaaban si wakupewa heshima na chuo, yule ni mtu wa kupewa heshima na taifa. kazi yake ya kusadikika ndio tuniona leo hii wakati yeye aliiona kabla ya tanu kuzaliwa! kazi zake tunazitumia mashuleni lakini sijui ni kwanini hatumpi heshima yake.

Shaaban Robert is my national hero.
 
kiukweli Shaaban Robert anatakiwa kupewa heshma kwani katoa mchango mkubwa ktk Elimu vile ukiangalia hata nchi za nje wanajifunza lugha hasa kupitia vitabu vya waandishi wetu kwanini wasipewe heshma ktk hli nimhimu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…