Vyuo vikuu vya Morogoro kufunga barabara kuu za Dar,Dodoma na Iringa ili kushinikiza kupewa Boom

Mpangawangu

JF-Expert Member
Joined
Mar 5, 2014
Posts
887
Reaction score
965
Serikali sikivu ya chama cha mapinduzi inaendelea kuwaadhibu watoto wa wakulima na maskini wa Tanzania wanaosoma vyuo vikuu kwa uchelewesha pesa za kujikimu.

Wamafunzi toka vyuo vikuu wa vya Jordan,Muslim university,na SUA,mpaka sasa hawana dalili za kupewa pesa za kujikimu(BOOM)ambazo kihalali zilipaswa kulipwa tarehe tano ya mwezi huu.

lakini kwa mujibu wa mawazili wa mikipo toka vyuo hivyo ,wamethibitisha kuwa hakuna dalili ya kupewa leo wala kesho kutokana na hazina kuwa hoi kipesa huku pesa za kuongeza posho za wabunge zikwa zinapatikana.

Sasa wanafunzi wanajipanga kufunga barabara zote tatu,

wale wa JORDAN wanajipanga kufunga barabara ya moro-Dar,MUM nao wanakusidia kufunga ile ya Dodoma -Moro ,huku Sua wakijiandaa kufunga barabara ya Iringa Dar.

mkakati huo wa kufunga barabara kuu ni kushinikiza kupewa hazi zao kwakuwa wanafunzi hawa wanaamini kuwa jaki haiombwi.

Pia wanadai kuwa serikali ya chama cha mapinduzi haifanyi mambo bila mashinikizo toka kwa watu ambao inawatawala.


My.take

Kama wamafunzi hawa watafanikisha hili,litakuwa pigo jingine kwa chama cha mapinduzi kwa kuwa watakwamisha uchumi wa nchi kutokana na umuhimu wa barabara hizo.

Mwigulu nchemba ,kazi ndio hiyooo imeanza,wasomi uliokuwa unajivunia kuwa nao kwenye mkoa maalumu wa vyuo vikuu morogoro wa ccm wamegoma kuendelea kuteswa na chama chako.

Tupe majibu kwa nini mnawatesa vijana hawa?
Au ni mbinu zenu ili wauze miili yao ili kujikimu kimaisha?

CCM imeshakosa uhalali wa kuendelea kuwatesa watanzania.
 
Kwanini waandamane wakati Serikali ya CCM ni sikivu? Au imekuwa je tena?
 
Wa Ud walitishia kunji jumatatu jumapili waka bandka majina ya kusaini boom walishapewa mda mpaka wamesahau
 
poleni madenti, kazeni buti watawapa tu. Sishangai sana nimepitia huko.
 
bora mgome....
chuo nnachosoma kimejaa inservice karibia robo tatu ya wanafunzi wote, hivyo mpaka saizi hamna hata dalili
 
Naona wanatafuta kichapo kutoka kwa polisi.

Wangeenda dodoma wakavunge barabara ya kuelekea bungeni sio kuwatesa wanachi wasio na hatia .

Sikubalian na hii tabia ya kuziba barabara wakati tukio/kero haihusian na maandamano au mgomo.
 
SUA hawawezi kugoma hawana huo mda, labda hivyo vyuo vya table marks(Jordan, Mum etc)
Isitoshe kufunga barabara ni kuingilia Wizara nyingine kabsa, kwanini wasigome tu Kusoma.?
Lakini pia hakuna shida tumejipanga pia tumepumuzika mda mrefu sana, watokee barabarani ili waone kazi ya tulivyo vionyesha kwenye Sherehe za Muungano. Tena nawatamani sana mnaojiita wasomi.
 
Kwani yulee mwakilishi wa ccm wa vyuo vikuu bw. Asenga hajapeleka malalamiko yenu kwa mwigulu? Hatari sana hii. Lengo lao watukamue wazazi ili tuhongeke kiurahisi 2015. Hebu wajipange kuwalipa haraka kwani hazina kuna hela nyingi tu alizozizcha kalasinga wa issue ya bilioni mia mbili.
 
mgomo unatisha udsm tu.wengine hawawezi.waonyeshe kuweza sasa
 

Acha ujinga unajua wana hali gani hao wanafunzi usiwe na mawazo ya kimbuzimbuzi.
 
namabari one eeeeee nambari one, nambari one ni sisem!!!!!!! WABUNGE tena wengine waganga wa kienyeji a.k.a wachawi 300,000/= KWA SIKU
MSOMI ANAYEHANGAIKA USIKU KUCHA KWA AJILI YA TAIFA HILI 450,000/= kwa zaidi ya miezi miwili!!!!!!!
Haya ni matusi. Watanzania tuamke tusinyonywe na hawa wakoloni weusi:israel:
 
Mbona jana niliona thread kuwa boom limetoka SUA au niliona vibaya?
 
Huu ni ujinga ilio pitiliza unaofanywa na wanafunzi wa vyuo vikuu. Mimi nawaita wanafunza. Ugomvi wenu na serkali yenu sikivu ya ccm mnataka muulete barabarani ili m disrupt biashara na starehe za wananchi wale wale wanaokwazwa na serkali hii sikivu ya ccm. ? mkifanya mgomo hakikisheni unawakwaza viongozi wenu wa ccm.
 
Hii ni kutokana na kucheweleshewa hela ya kujikimu wawapo hapo chuoni....hvyo gvt imetakiwa kutoa majina watu wasaini..nawasilisha
 

unafikiri kupitia mat...k.nyie ndo mnafaidi nch hii na baba zenu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…