Vyuo vikuu vya tanzania vingine viige mfano huu!

Kubingwa

JF-Expert Member
Joined
Apr 23, 2010
Posts
505
Reaction score
69
Nimekuwa nikijiuliza muda mrefu sana kwa nini vyuo vikuu vya Tanzania havina matawi yake ktk nchi za Africa Mashariki ingali huku Serikali ya Tanzania ikiwahimiza Watanzania kuchangamkia fursa za ajira wakati hata vyuo vikuu vyake vinashindwa kuwa na matawi katika nchi za Afrika Mashariki.
Wenzetu Kenya na Uganda wamejitahidi kuchangamkia fursa ya kielimu kwa kufungua matawi ya vyuo vyao vikuu.
Mfano Kampala University wana tawi Dar es Salaam na Jomo Kenyatta University wana tawi lao Arusha.

Na hatimaye Open University of Tanzania (OUT)hatimaye wamevunja ukimya nadhani wana tawi Nairobi maana nimeona tangazo lao kupitia Citizen Tv ya Kenya kwa kushirikiana na Institute of Human Resource Management cha Kenya.
Vyuo vingine vinangoja nini au ndo ukiritimba?
Vyuo vikuu vingine vya Tanzania muige mfano huu.
 
Umesema jambo la uhimu sana ndugu imefika wakati viongozi wa vyuo waache ukiritimba,wanafuzi wakidai mikopo yao wanafukuzwa,madaktari wanafuzi wakiomba stahili zao wanafukuzwa na wagonjwa wanapoteza maisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…