Jamani naomba tusaidiane mawazo labda mi sielewi vyema. Ni kweli kuwa vyuo vingi vya ualimu vya serikali mtu akiteuliwa kuwa principal anakuwa amepewa mrija wa kuvuta utajiri ingawa nahisi wanashirikiana na maofisa wa wizara ya elimu. Mfano mzuri ni lile sakata la chuo cha Korogwe.
Sasa chuo kingine ambacho inabidi kimulikwe vyema ni chou cha ualimu cha Mhonda kilichoko mkoani Morogoro. Nimesomesha mtoto pale lakini kila mwaka michango ni mingi na inazidi ada. Mwezi wa Dec 2013 wanachuo walipoenda likizo, walikuja na barua zinazoonyesha baadhi ya michango kama vile, Ukarabati 20000, ujenzi 25000 na mambo mengine lukuki. Principal akawapa na fomu ya kuchangisha watu michango kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za ibaada, jambo ambalo ni jema. Kila mwanafunzi aliambiwa achangishe 25000 na kuendelea. Maana ya mchango wa kwenye fomu ninavyoelewa ni hiari ya mtu. Leo hii vijana wanamaliza mtihani, Principal amewageuka na kuwanyima vyeti vya Leaving kwamba mpaka walipe hiyo 25000 ambayo walipaswa wapitishe fomu kwa watu wawachangie. Je hii ni halali?
Je wizara ya elimu na katibu mkuu mlibariki swala hili?
je wabunge wetu mnajua kuwa vyuoni huko ufisadi upo?
Zaidi ya hapo wanafunzi hawahawa wamesombeshwa mawe nakufyatua tofali za kutosha kwa ajili ya ujenzi wa madarasa na nyumba za walimu pamoja na hizo nyumba za ibada.
Mi sidhani kama ni sahihi tumhurumie mtoto wa maskini nae anahtaji elimu na kuajiriwa.
karibu wadau kwa mjadala