Vyuo visivyotambuliwa ndio vyuo gani?

Vyuo visivyotambuliwa ndio vyuo gani?

Jembemtaji

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2014
Posts
1,193
Reaction score
926
Mara nyingi zinapotoka nafasi za kazi hasa zile zinatangazo Serikali. Kunakua na kukusisitiza waombaji wawe wametoka kwenye vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.

Sasa najiulizaga maswali sipati majibu

1. Vyuo ambavyo havitambuliwi na serikali ni vipi?
2. Kama havitambuliwi mbona wanatambua kua kuna vyuo havitambuliki?
3. Wasomi wa vyuo hivi ni akina nani na wanasoma kwa malengo gani?
4. Ina maana hakuna shida kumiliki au kusoma chuo kisichotambulika na Serikali?

Ni hivyo tu wadau nahitaji mwanga.
 
Kunaa tu chuo uchwara huwaa tupo mtaaan majengo kama secondary za kata huwa havina usajil ilaa wana offer courses na kudaili wanafuz kadhaaa. Kumbuka chuo kilitangazwa na ITV nmesahau mwez kipo MUSOMA huko mmuliki anatembea na wanafunzi na kilikuwaa na only 20+ students all courses
 
Makamu mkuu wa chuo cha Sokoine University of Agriculture (SUA) alinifungua macho hapo juzi kwenye sherehe: namnukuu "Tanzania chuo kikuu bora kinachotambulika kwa tafiti bora ndani na nje ya nchi ni SUA, vingine vyoooote havitambuliki". Mwisho wa kunukuu!

Nadhani umepata jibu hapo.
 
Kimojawapo zion

Sent from my Infinix X624B using JamiiForums mobile app
Zion kina usajili.

Sema kuna vyuo janja janja, kinasajiliwa kutoa taaluma fulani halafu kinaanza kutoa taaluma ambayo hakikusajiliwa.

Mfano ukisoma Nursing huko Amazon College sidhani kama utatambulika.

Kampala University waliwahi kufanya huu mchezo na waluwaumiza watu wengi sana.
 
Sasa kwanini vinaruhusiwa kufanya kazi??
Makamu mkuu wa chuo cha Sokoine University of Agriculture (SUA) alinifungua macho hapo juzi kwenye sherehe: namnukuu "Tanzania chuo kikuu bora kinachotambulika kwa tafiti bora ndani na nje ya nchi ni SUA, vingine vyoooote havitambuliki". Mwisho wa kunukuu!

Nadhani umepata jibu hapo.
 
Sasa mbona vinaendelea na kazi wakati serikali haivitambui.
Vyuo ambavyo havisajiliwa na NACTE au TCU

Kwa mfano mitaani Kuna vyuo madrasa vipo ila havijasajiliwa kutoa taaluma fulani
 
Vyuo Vingi ni below standard. Graduate wa "pass" eti ndiye lecturer, wapi na wapi? If you want a cream profession go to:
UDSM, SUA, MUHAS only! You will be recognized worldwide
 
Back
Top Bottom