Vyuo vya Ualimu na Diploma feki

Captain22

JF-Expert Member
Joined
Aug 25, 2011
Posts
629
Reaction score
282
Wakuu nawasalimu wote na natumaini week end inamalizika vyema.
Miaka ya hivi karibuni kumekuwa na ongezeko kubwa sana la "utitiri" wa vyuo binafsi vinavyotoa elimu katika fani mbalimbali ikiwemo fani ya Ualimu.
Kumekuwa na vyuo vinavyojitangaza katika media mbalimbali kuwa vinatoa mafunzo ya ualimu katika ngazi za cheti na diploma katika fani ya ualimu wa shule za "English Medium". Nitapata shida kuufahamu huu ualimu wa English medium ni upi hasa. Je wizara ya elimu inautambua huu ualimu wa english medium? Syllabus ya huu ualimu tofauti yake na ualimu wa kawaida ni ipi?Kama wizara ya Elimu haiutambui huu ualimu unaoitwa wa English medium je ni kwa nini vyuo hivi viendelee kuwadanganya watanzania haswa wazazi wenye nia ya dhati kabisa ya kuwaendeleza watoto wao?
Mbaya zaidi hao wanafundishwa ualimu huu uliobatizwa ualimu wa English medium ni wale wasiokizi vigezo vya kufanya mafunzo ya ualimu kwa kutokuwa na alama zinazotakiwa na wizara ya Elimu. Please vyombo vinavyohusika zilitazame jambo hili ambalo mbali ya kuwadanganya wazazi na wanafunzi wenyewe, linaondoa hadhi ya fani ya ualimu na kudidimiza elimu ya taifa hili.
Nawasilisha tujadili kwa ukweli dhati na kina kwa maendeleo yetu.
 
Na mbaya zaidi wakimaliza hawaajiriwi na serikali, sijui serikali inalichukuliaje hlo. Kuna rafk yangu mmoja anasoma kwenye chuo kama hicho mkoani K/njaro.
 
Na mbaya zaidi wakimaliza hawaajiriwi na serikali, sijui serikali inalichukuliaje hlo. Kuna rafk yangu mmoja anasoma kwenye chuo kama hicho mkoani K/njaro.

sasa umeshaambiwa ni ualimu wa english medium sasa serikal kwani ina hizo shule'? Mpaka iwaajiri??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…