proff g
Senior Member
- Jul 16, 2016
- 146
- 113
Mwaka wa masomo 2024/2025 umekuwa wa tofauti kuliko miaka nyumba, kupitia wizara ya Elimu kumekuweko na mabadiliko ya kimitaala katika uendeshaji wa Elimu yetu. Moja ya madiliko ni kuwekwa Kwa vigezo vinavo fanana Kwa ngazi tofauti mfano nihili la vyuo vikuu na vyuo vya ualimu kuwa na vigezo sawa kwenye kufanya maombi. Inawezekana likawa ni jambo zuri lakini hofu nikuwa linafanyiwa majaribio kwenye maisha ya watoto masikini wa kitanzania, ukizingatia tayari tumenza kuona changamoto za uendeshaji wa mabadiliko wa sera mpya hii ya Elimu mfano kusitishwa Kwa utekelezaji wa sera Kwa kidato cha Tano, je Bado tunasubiria tuone kama huku vyuoni pia kutokee changamoto, mh Raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania ipoa haja ya kulifuatilia hili kiundani tofauti litakwenda kuumiza watoto wa masikini