Jf mods tufanyieni msaada tusome vizuri hili tangazo yani likuzwe kidogo.
Mods wapo likizo:
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
Simu: 022-2110146/2110150/2, 211679, Faksi: 022-2113271,
Tovuti:
United Republic Of Tanzania - Ministry of Education and Vocational Training
TANGAZO LA NAFASI ZA MAFUNZO YA UALIMU NGAZI YA CHETI KWA MWAKA WA MASOMO 2014/2015
UTANGULIZI
Moja ya mikakati ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi katika kuandaa walimu mahiri ni pamoja na kuhakikisha kuwa wanafunzi wanaochaguliwa kujiunga na mafunzo ya ualimu ngazi ya Cheti ni wale wenye ufaulu mzuri katika mtihani ya kidato cha NNE. Ili kufanikisha azma hii, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi itadahili wanafunzi wenye ufaulu wa Daraja la Tatu kwa ajili ya Cheti na wenye ufaulu wa alama 26 au 27 (mwaka 2004 hadi 2012) na alama 33 au 34 (mwaka 2013) watadahiliwa katika programu ya mafunzo kabilishi ya mwaka mmoja.
Aidha, kipaumbele katika udahili kitatolewa kwa waombaji waliofaulu masomo ya
Sayansi, Hisabati, English na Kiswahili. Watakaojiunga na mafunzo ya ualimu na kufaulu mafunzo yao watapatiwa ajira moja kwa moja kulingana na taratibu za Serikali.
VIGEZO
Vigezo vifuatavyo vitatumika kuchagua wanachuo wa kujiunga na mafunzo ya ualimu mwaka 2014/15.
1: MAFUNZO YA UALIMU TARAJALI NGAZI YA CHETI DARAJA 'A':
MUDA MIAKA 2
(i) Cheti Ualimu wa kawaida katika vyuo vya Ilonga, Kabanga, , Kitangali, Mandaka , Murutunguru , Ndala , na Tarime.
(ii) Cheti Ualimu Elimu ya Awali katika vyuo vya Kabanga, Kinampanda, Mhonda, Mtwara (U), Singachini, Tandala, Tarime
(iii) Cheti Ualimu Elimu kwa michezo katika vyuo vya Ilonga, Tarime, Ndala na Mtwara (U)
Mwombaji awe:
Mhitimu wa Kidato cha IV kati ya mwaka 2004 na 2013 mwenye ufaulu wa kiwango kisichopungua
Daraja la III katika Mtihani uliofanyika katika kikao kimoja.
MAFUNZO KABILISHI NGAZI YA CHETI (BRIDGING COURSE) KWA
2: AJILI YA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA UALIMU NGAZI YA CHETI:-
MUDA MWAKA 1
Mafunzo katika vyuo vya ualimu Bustani, Kinampanda, Mhonda, Mpuguso, Mtwara (U), Nachingwea, Singachini, Tandala, Katoke na Sumbawanga.
1.
Mwombaji awe:
(i) Amehitimu wa Kidato cha IV kati ya mwaka 2004 hadi 2012 na awe amefaulu kwa kiwango kisichopungua
Daraja la IV kwa alama 26 au 27 (kwa mtihani wa mwaka 2004 hadi 2012) na
alama 33 au 34 (mtihani wa mwaka 2013) kwa mitihani iliyofanyika katika kikao kimoja; na
(ii) Mwenye ufaulu wa angalau kiwango cha D katika masomo ya Sayansi, Hisabati, English na Kiswahili katika Mtihani wa Kidato cha IV.
Tanbihi: Watakaofaulu mtihani wa mafunzo rekebishi wataendelea na mwaka wa pili wa mafunzo ya ualimu ngazi ya cheti Daraja A
3: ELIMU MAALUM: MIAKA 2 katika chuo cha Patandi:-
Mwombaji awe:
(i) Mwalimu wa Daraja 'A' mwenye uzoefu wa kazi ya Ualimu kwa muda usiopungua miaka miwili.
(ii) Mwenye ufaulu angalau somo moja la Sayansi katika Mtihani wa Kidato cha IV.
Tanbihi:Walimu wanaofundisha Elimu Maalum hata kama hawana mafunzo maalumu ni sifa ya nyongeza (uthibitisho uambatishwe).
MAELEZO MUHIMU
(i) Vigezo vilivyoelekezwa kwa waombaji wa mafunzo ya Ualimu ngazi ya Cheti ni kwa ajili ya waombaji wa mafunzo ya Ualimu katika
Vyuo vya Ualimu vya Serikali na visivyo vya Serikali;
(ii) Muombaji wa chuo cha ualimu cha Serikali anatakiwa kuchagua vyuo visivyopungua vitano ambavyo angependa kujiunga navyo akianzia kile anachokipendelea zaidi;
(iii) Wahitimu Kidato cha IV mwaka 2013 waliojaza nafasi ya mafunzo ya Ualimu ngazi ya Cheti Daraja 'A' kwenye '
Selforms' wakati wanamaliza Elimu ya Sekondari
wanatakiwa kuomba upya mafunzo hayo;
(iv) Waombaji wa mafunzo ya Ualimu walioajiriwa watakaopatiwa nafasi za mafunzo watapaswa kupata ruhusa (Release) kutoka kwa waajiri wao;
(v) Majibu kwa watakaochaguliwa kujiunga na mafunzo ya Ualimu katika vyuo vya Serikali yatatolewa kwenye Tovuti za Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi (
United Republic Of Tanzania - Ministry of Education and Vocational Training), OWM-TAMISEMI (
PMORALG | Prime Minister's Office - Regional Administration and Local Government) na NACTE (
The National Council for Technical Education)
(vi) Waombaji watakaochaguliwa watatumiwa barua za kujiunga na mafunzo na Wakuu wa vyuo vya Ualimu watakakokuwa wamepangwa kupitia anuani zao;
(vii) Tangazo hili lipo pia katika tovuti ya OWM TAMISEMI:
www.pmoralg.go.tz na NACTE:
www.nacte.go.tz na kwenye ofisi za Makatibu Tawala (M) na vyuo vya ualimu
.
Namna ya kutuma maombi:
a) Waombaji watume maombi yao kwa njia ya
MTANDAO (online application) kupitia tovuti zifuatazo:
www.moe.go.tz AU
The National Council for Technical Education
2. Maombi kwa njia ya mtandao yataambatana na ada ya
shilingi 10,000 itakayolipwa kwa kutumia
MPESA. Maelekezo ya kina kuhusu namna ya kutuma maombi kwa njia ya mtandao yanapatikana katika tuvuti ya wizara
United Republic Of Tanzania - Ministry of Education and Vocational Training na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi
The National Council for Technical Education
Malipo ya maombi yanaweza kufanyika kupitia M - PESA kama ifuatavyo:
1. Piga *150*00#
2. Chagua 4. (Lipa kwa MPESA);
3. Chagua 1. (Weka LIPA Namba);
4. Weka LIPA Namba (ingiza namba
607070);
5. Ingiza kiasi (ingiza kiasi cha 10,000.00);
6. Weka Enter Reference No. ( ingiza
1234);
7. Weka namba ya SIRI (ingiza namba yako ya siri); na
8. Ingiza 1 kuthibibitisha malipo.
AU
b) Barua kwa:
KATIBU MKUU
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
S.L.P. 9121
DAR ES SALAAM (Aione: Mkurugenzi, Elimu ya Ualimu)