Lugha zina namna tofauti ya kutaja majina ya nchi, waingereza wanaiiita Swidi Sweden, waswahili wanaiita Swidi, Waswidi wenyewe wanaiita nchi yao Sveridge.
Waingereza wanaiita Fini Finland, waswahili wanaiita Fini, wafini wenyewe wanaiita Suomi.
Waingereza wanaiita Marekani (US) America, waswahili wanaiita Marekani, wamarekani wenyewe wanaiita America.
Kusema watu wa Msumbiji hawalijui jina hilo ni sawa na kusema wamarekani hawalijui jina la "Marekani".
Msumbiji ni jina la Kiswahili la Mozambique, unless mtu anajua Kiswahili au kawasikia wanaoongea Kiswahili wakiitaja hii nchi kwa jina hili, anaweza asilijue.
Kama vile Marekani lilivyo jina la Kiswahili na Mmarekani asiyejua kiswahili na kutopata nafasi ya kuwasikia wanaoongea kiswahili wakisema nchi yake kwa jina hili, hatajua, rightly so.