Wa-Olmec, Mpango wa Kuharibu Ukuu wa Watu Weusi (Waafrika)

TL. Marandu

JF-Expert Member
Joined
Jul 12, 2015
Posts
3,625
Reaction score
5,810
Ukitaka, Kunyonga Jamii, Kwamba wanawezaje Kuendeleza Maisha, Uvumbuzi na Elimu na Utamaduni wao? Basi Haribu historia yao. Bila Kujua Historia, Bila Kujua tulikuwa Kina nani, na tulifanya tulitoka wapi? Ni Vigumu Kujua Kuwa sisi Twaweza Kuwa akina nani na Tunakokwenda ni wapi.

Jitihada Kubwa sana, simefanyika Kujitahidi sana Kuondoa Katika Historia, Ukuu na Mafanikio ya Jamii za Watu weusi. (Tena tuondokane na Kufikiri watu weusi walikuwa waafrika tu) Njama hizi za Kuharibu Ushahidi wa Ukuu wa Mtu mweusi haujaanza zamani sana. Kabla ya Biashara ya Utumwa, Hakukuwa na Tabia ya Watu waliojiona ni bora au ni duni kwa sababu tu ya Rangi ya ngozi zao au nywele zao.

Mara Biashara ya Utumwa ilipoanza na Kushamiri, na Kisha Kufuatiwa na Ukoloni, Basi zikaanza jitihada za Watu wa Kishetani, Watu wenye Kukera sana walioingiza wazo batili kuwa watu wa mbari fulani walikuwa sio watu halisi, au hawakuwa watu wenye ustaarabu. Na Bahati mbaya sana Miaka ya mwishoni ya 1800, Afrika ilishadidimizwa sana kutokana na Vitisho vya Biashara ya Utumwa watu walijificha Misituni kwa sababu ya kuhofia Kukamatwa. Ikumbukwe haikuwa kwa siku mbili bali miaka karibu 500, kuanzia 1360 Utumwa Ulipoanza mpaka walipokuja. Haichukui miaka hata 20 Kuharibu jamii iliyo katika hofu. Mfano mzuri ni Iraq Vita vilivyodumu miaka 13, imeharibu kabisa maisha yao au Libya ilivyoharibiwa chini ya miaka 5, Unaweza Kujua adhari za Vitisho vya Miaka 500.

Hivyo Utamaduni wa Mtu mweusi, Elimu, Lugha, Uwezo wa Ugunduzi, Uliharibiwa Kabisa. Mimi naamini kama Utumwa na Ukoloni usingekuwepo. Uchumi , Maendeleo na Technologia katika nyanja zote kwa watu weusi Ungekuwa sawa na wengine, kwa kuwa Hatuko sayari Nyingine.

Kinachoudhi Kuliko vyote, Ni kuwatenga Weusi na Ukuu wa Historia yao, Kama vile madai Kuwa Mafaraoh wa Misri hawakuwa weusi. Au Kujifanya Kutozungumzia Kabisa Ugunduzi wa Kihistoria Unaomhusu Moja kwa Moja mtu mweusi.

Mfano Ugunduzi huu hausemwi sana na Wangelikuwa na Uwezo wa Utashi wangepiga bomu na Kuharibu Kabisa isije Kujulikana Mtu mweusi anahistoria na alifikia Mambo makuu!
 
Ninachojua tajiri mkubwa kuliko wote katika miaka 2000 iliyopita ni Mwafrika mfalmw Mansa Musa wa dola ya Mali, thamani ya utajiri wake ni dola bilioni 400 ambazo Warren buffet na Billgates wanasubiri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…