Wa Tz Kila Siku tunalaumu Makocha...

ibanezafrica

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
7,261
Reaction score
6,553
Marcio Maximo pamoja na yote akatimuliwa,kutoka hapo umepita mlolongo mrefu wa makocha..wazawa na wageni wote wameonekana hawafai....
Sasa wiki hii nayo gumzo lililopo ni kua eti kocha wa Azam na kocha wa Yanga wote hawafai ! Ikumbukwe kocha wa zesco akishawahi kutumika hapa nchini lakini alionekana hamna kitu,lkn majuzi kapata angalau sare ugenini...
Cha kujiuliza Tanzania tunataka kocha wa aina gani ? Awe malaika ? Kwanini tunaukwepa ukweli kuwa Tanzania soka hatuliwezi ? Klabu zetu sasa zinategemea wachezaji wa kigeni.basi kwanini tunashindwa kuhoji uwezo wa wachezaji wetu wazawa ?Okwi anaondoka nchini baada ya miaka mitatu anarudi bado anaonekana kwetu ana kiwango bora ! Hicho wanachokikosa wachezaji wetu ndio tatizo kubwa la soka letu kuanzia vilabuni hadi taifa.
Serikali isimamie hili kwa hakika vinginevyo tutabakia hapa tulipo miaka nenda rudi.
 
Kwa hiyo hata Amunike naye umemuweka kwenye kundi hilo hilo! Yaani anapanga timu nzima wachezaji wa ulinzi, timu inafungwa kwa kushindwa kushambulia halafu tuwalaumu wachezaji tu?

Sikatai wachezaji kuhusika kwa baadhi yao kushindwa kujitambua, viongozi wa vilabu kuendekeza siasa, serikali kukosa sera nzuri ya michezo, lakini hata makocha hawawezi kukwepa lawama.
 
Tz hata aje kocha gani bado atalalamikiwa tu.
 
simba walimkataa dylan kerr akaenda Gor mahia leo hii simba sc wanagombania wachezaji kina kahata na kagere waliojengwa na kutengenezwa na huyo huyo kocha dylan kerr hao ndiyo wabongo!
 
Ujue amunike ni mkufunzi wa fifa programu za vijana...
Je nini tatizo letu ? Maana wazi tunajua wazi timu zetu hazitafika mbali si klabu si taifa stars
 
Hakuna kitu tunachoweza zaidi ya ujuaji na porojo nyingi bila vitendo. hao makocha nivisingizio tu ila ukweli tatizo nisisi wenyewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…