Waache waende kutafuta wa zaidi yako ila usikubali warudi tena kwako endapo watamkosa

Mwanasayansi Kalivubha

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2024
Posts
344
Reaction score
926
WAKIKUKOSA WALIPOENDA KUKULINGANISHA USIKUBALI WARUDI TENA KWAKO.

Ukiona mtu karudi kwako tena usishangalie bali jiulize haya:
#Kwanini aliondoka?
#Kwanini karudi tena?
#Wewe si yule yule?

KWANINI ALIONDOKA?

Ukweli mchungu huwa :
#Alikuona sio hadhi yake.
#Alijua wapo wa zaidi yako
#Hali yako haikuwa rafiki kwake.
#Hakuwa na upendo kwako.
#hukumfaa .

KWANINI ARUDI?
#Alipoenda akijua ni zaidi yako kakuta sio.
#Kufukuzwa hivyo ili asikose pakwenda karudi kwako.
#Aliyempata kamuumiza kiasi cha kumpa majuto ndio maana kakukumbuka.

UFANYE NINI?

#Msamehe ila sio lazima umpe tena nafasi ya pili
#Akirudi akute unaendelea na maisha yako na sio kumsubiri yeye .
#Usikubali kuwa mtu wa kurudiwa kirahisi baaada ya kuachwa.

#Instagram @fikia ndoto zako.
 
Asante sana mkuu, umenena maneno ambayo yamegusa maisha ya vijana wengi ambao wameanza kujitafuta.

Wengi wao kwa umri huo wanatamani kupata wenza wa kuwafariji kuwapa amani na utulivu ila wanaishiwa kusalitiwa, baada ya muda wenza wao wanarud kuwaomba msamaha na wanawasamehe. Hili ni kosa kubwa ktk mahusiano japo wachache wanaweza wakawa wamebadilika kweli kweli.
 
Kweli kabisa mwalimu
 
Hii ilinitokea soon baada ya kumaliza chuo akaenda kwa LECTURER mi nikaachwa, katumiwa huko baada ya kuwa dumped anarudi ku-apologize. Na amenikuta siishi kinyonge kama before. NEVER BACK OFF.
 
Akirudi ukampokea tafsiri yake ni kuwa kakuchukulia wewe kama nyama ya nyongeza.
 
Wengine ndio principle zetu, ukiniacha naendelea na safari, hutanikuta uliponiacha
 
Back
Top Bottom