Waacheni watoto wadogo waje Kwangu

Waacheni watoto wadogo waje Kwangu

ikigijo

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2017
Posts
1,839
Reaction score
1,902
Habari wadau,
Hivi Yesu Krisu alipokuwa anawaambia wanafunzi wake/Watu kuwa:
"Waacheni watoto wadogo waje kwangu kwa maana ufalme wa mbingu ni wao"
Je?
1.Kwani walizuiliwa Kwenda kwa Yesu?
2.Kwanini Ufalme wa mbingu ni wa watoto wadogo? Wakubwa Je?
3.kwanini wametolewa mfano wa watoto wadogo wakati kila MTU anakuwa mdogo na kuna wakati anakuwa Mkubwa.
Karibuni kwa mawazo Great thinkers!
 
Watoto wadogo wakikuamini hawana unafiki wala kwa nini kwa nini nyingi.
Hata akiwa juu ya bati ukimwambia ruka nitakudaka ataruka.

Watu wazima wanatakiwa kumuamini Mungu katika viwango vya watoto wadogo.
Total undivided trust.
 
Soma kitu kimoja kiitwacho "ego"

Kiswahili chake sikijui,
Hicho ndio chanzo cha dhambi zote duniani,
Mtu akiishinda ego ameishinda dhambi,

Watoto wadogo baadhi yao lakini sio wote hua ktk hali ya utakakatifu kwa sababu wanakua hawajatenda dhambi,

Yesu ni mtu pekee aliyeweza kuishinda ego,
Ndio maana aliweza hata kutembea juu ya maji,
Kuvumilia maumivu ya misumali mikononi na miguuni bila kutukana au kutusaliti sisi,
Hii ni kwa sababu alielewa ego jinsi inavyo fanya kazi,

Hivyo basi aliposema waacheni watoto wadogo waje kwangu alikuwa anaeielewa formula vizuri sana.
 
Back
Top Bottom