Waafrica katika District 9

Chapakazi

JF-Expert Member
Joined
Apr 19, 2009
Posts
2,874
Reaction score
316
Jamani ni lini Waafrica tutaacha kudhalilishwa katika movies? Leo nimebahatika kwenda kuangalia hii movie mpya - District 9. Imekuwa based katika jiji la Johanesburg. Kwa ujumla ni movie nzuri (good message), lakini kilichoniudhi ni roles walizopewa Waafrica. Sijaona Mwaafrika yeyote aliyekuwa katika position kubwa kwenye movie. Yani kwanza sisi ndo tumepewa role ya kuishi pembeni mwa Aliens. Na kwenye movies wanaonyesha hadi machanguduo wa kiafrica wanaofanya mapenzi na hivyo viumbe! Nilipokuwa ndani ya cinema nilitamani kutoka, hasa ukikusudia kuwa nilikuwa Mwafrika peke yangu.

Ni mpaka lini tutaendelea kuchukuwa roles za kipumbavu na za kujidhalilisha? Hii inajenga pyschological effect. Hasa ukifikiria kwa hawa wazungu waliozaliwa huku na kukulia huku, basi wanabaki na image mbovu ya Africa. Kweli inabidi tuombe wabadilishe hali hii ama sivyo tugome ku-act katika hizi movie zao za udhalilishaji.
 
Hasa Waswahil wamehusishwa, eti 'Mambo powa....'
 
si ndo hapo nilishangaa na huku walishasema wale ni Nigerians!!
 
Maendeleo:
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…