Waafrika tunalazimishwa kuwategemea wazungu?

Waafrika tunalazimishwa kuwategemea wazungu?

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
21,470
Reaction score
40,593
Kwanini kama inaonekana waafrika Kila wakati tunalalamika kuhujumiwa na wazungu hasa Marekani?

Je, Afrika tuna mkataba na Marekani/wazungu kuwa ni lazima tuwategemee wao kuthibitishwa, kiuchumi, kijeshi na kijamii?
 
Tatizo la waafrika ni kushindwa kujisimamia kwa kukosa hulka ya uongozi ndio maana kila siku wao ni kutafuta tu mchawi kwa matatizo yao wanayojiletea wenyewe.

Hapa Tanzania kila mwaka bajeti inapitishwa na bunge na baada ya hapo tu watumishi wa serikali na hata na wabunge wenyewe huingia kwenye ligi kali ya kutafuna fedha hizo na ushahidi waga upo kwenye ripoti ya CAG ya kila mwaka lakini hakuna aliyewahi kuchukuliwa hatua yoyote hadi imekuwa ni mazoea.!!!

Ccm wenyewe siku zote wanachofanya ni kuhakikisha kwamba piga ua wako madarakani ila hawana programu yoyote ya maendeleo kwa nchi hii na hawatakaa wawe nayo. Never.
 
Back
Top Bottom