Waafrika tunazaliana sana halafu kuumudu uzao huo tunategemea misaada ya wazungu: Ni aibu maana hatuna tofauti na mbuzi kwenye zizi

Waafrika tunazaliana sana halafu kuumudu uzao huo tunategemea misaada ya wazungu: Ni aibu maana hatuna tofauti na mbuzi kwenye zizi

Rorscharch

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2013
Posts
878
Reaction score
2,014
Takwimu zinaonyesha tofauti kubwa katika ukuaji wa idadi ya watu kati ya nchi za Afrika Mashariki na zile za Scandinavia kati ya mwaka 1960 na 2024. Hapa chini ni muhtasari wa mabadiliko hayo:

Afrika Mashariki:

Kenya:
8.1M (1960) → 54.7M (2024)

Tanzania: 10.1M (1960) → 67.8M (2024)

Uganda: 6.9M (1960) → 48.6M (2024)

Rwanda: 2.9M (1960) → 13.6M (2024)

Burundi: 2.6M (1960) → 13.2M (2024)

Scandinavia:

Sweden:
7.5M (1960) → 10.5M (2024)

Norway: 3.6M (1960) → 5.5M (2024)

Denmark: 4.6M (1960) → 5.9M (2024)

Mtazamo wa Kijamii: Kujaza Dunia kwa Wingi au Maendeleo?

Hivi ni busara kweli kuzaliana kiholela halafu kuishi kwenye ufukara wa kutisha? Hivi, mnazaliana kama panya kisha mzungu aje abebe mzigo wa matatizo yenu? Hata aibu hamuoni?

Wakati nchi za watu zinaongeza idadi ya watu kwa tahadhari, nyinyi mnashindana kuzijaza ardhi zenu na watu wasio na ajira, elimu wala huduma za msingi. Ni ajabu: watoto wanazaliwa kwa wingi, lakini nani anawalea? Serikali zenu zinakopa kila siku ili kujenga shule, hospitali, na hata kutoa ruzuku ya chakula, lakini bado hamjachoka kuongezeka kama mchwa.

Halafu, huyo huyo mzungu mnayemlaumu eti analeta UKIMWI kuwaangamiza Waafrika, ndiye anayegaramia ARV zenu bure. Mnadai anataka kuwapunguza, lakini ndiye anayewaletea chanjo za kuokoa maisha ya watoto wenu! Unafiki huu mnautolea wapi?

Ni kawaida Afrika: nchi yenye watu milioni 10, lakini ni milioni 2 tu wanaolipa kodi, huku 8 zilizobaki ni mizigo. Matokeo? Serikali inazungusha bakuli kila kona, kuomba misaada kutoka kwa waliowazidi maarifa. Na cha kushangaza, mkishasaidiwa, mnawageuka wahisani wenu na kuanza kuwatuhumu kwa uchawi na njama za kuwateketeza.

Kwa mtindo huu, kweli tuna mpango wa kujikwamua au tunaishi kwa mtazamo wa “vizazi vifuatavyo watajijua”?
 
Unaweza kukuta wakati unaandika uzi huu ulikuwa umetoka kupokea text ya mchepuko wako anakueleza kuwa alitapika vidonge vya P2, Haiikufanya kazi, so anahisi ana mimba yako.

Anywayz, ahsante, over-population ni hatari.
 
Kwahiyo tusizae na wanaume kwa wanaume tuoane kama wazungu kisa tu maskini?

Pumbavu.
 
Kwahiyo tusizae na wanaume kwa wanaume tuoane kama wazungu kisa tu maskini?

Pumbavu.
Zaa ila huyo mtoto hadi awe mtu mzima afike hapo sio kwa msaada wa watu wa Marekani

Sio picha inaanza tu unaanza kulalamika kwa RC Chalamila kwamba hospitali imemlipisha mkeo 50,000/- kwa kujifungua
 
Takwimu zinaonyesha tofauti kubwa katika ukuaji wa idadi ya watu kati ya nchi za Afrika Mashariki na zile za Scandinavia kati ya mwaka 1960 na 2024. Hapa chini ni muhtasari wa mabadiliko hayo:

Afrika Mashariki:

Kenya: 8.1M (1960) → 54.7M (2024)

Tanzania: 10.1M (1960) → 67.8M (2024)

Uganda: 6.9M (1960) → 48.6M (2024)

Rwanda: 2.9M (1960) → 13.6M (2024)

Burundi: 2.6M (1960) → 13.2M (2024)

Scandinavia:

Sweden: 7.5M (1960) → 10.5M (2024)

Norway: 3.6M (1960) → 5.5M (2024)

Denmark: 4.6M (1960) → 5.9M (2024)

Mtazamo wa Kijamii: Kujaza Dunia kwa Wingi au Maendeleo?

Hivi ni busara kweli kuzaliana kiholela halafu kuishi kwenye ufukara wa kutisha? Hivi, mnazaliana kama panya kisha mzungu aje abebe mzigo wa matatizo yenu? Hata aibu hamuoni?

Wakati nchi za watu zinaongeza idadi ya watu kwa tahadhari, nyinyi mnashindana kuzijaza ardhi zenu na watu wasio na ajira, elimu wala huduma za msingi. Ni ajabu: watoto wanazaliwa kwa wingi, lakini nani anawalea? Serikali zenu zinakopa kila siku ili kujenga shule, hospitali, na hata kutoa ruzuku ya chakula, lakini bado hamjachoka kuongezeka kama mchwa.

Halafu, huyo huyo mzungu mnayemlaumu eti analeta UKIMWI kuwaangamiza Waafrika, ndiye anayegaramia ARV zenu bure. Mnadai anataka kuwapunguza, lakini ndiye anayewaletea chanjo za kuokoa maisha ya watoto wenu! Unafiki huu mnautolea wapi?

Ni kawaida Afrika: nchi yenye watu milioni 10, lakini ni milioni 2 tu wanaolipa kodi, huku 8 zilizobaki ni mizigo. Matokeo? Serikali inazungusha bakuli kila kona, kuomba misaada kutoka kwa waliowazidi maarifa. Na cha kushangaza, mkishasaidiwa, mnawageuka wahisani wenu na kuanza kuwatuhumu kwa uchawi na njama za kuwateketeza.

Kwa mtindo huu, kweli tuna mpango wa kujikwamua au tunaishi kwa mtazamo wa “vizazi vifuatavyo watajijua”?
Mkuu,

Nilikuwa nasoma kitabu cha Profesa Paul Bjerk, kinaitwa "Building A Peaceful Nation : Julius Nyerere And The Establishment if Sovereignty In Tanzania 1960 -1964".

Katika kitabu hicho, moja ya vitu nilivyojifunza ni kwamba, serikali ya Tanganyika na halafu Tanzania, kuanzia mwanzo kabisa baada ya Uhuru wa Tanganyika, ilikuwa na ari kubwa sana ya kuleta maendeleo. Ikaanza kwa mpango wa maendeleo wa miaka mitano wa kwanza kabisa. Ikapanga maendeleo mengi sana, kujenga madarasa watoto wasome, mambo ya afya, etc.

Baada ya miaka mitano, serikali ikarejea kuangalia ufanisi wa mipango yake.

Serikali ilijikuta kuwa, ingawa imefanikisha mipango yake kama ilivyopanga, bado kulikuwa na pengo kubwa sana kimaendeleo, kwa sababu, idadi ya watu iliongezeka sana, ikawa ingawa mahitaji yaliyopangwa kufikiwa yalifikiwa, mahitaji mapya yakazidi kwa kiasi kikubwa sana mahitaji ya zamani. Planners wa serikali hawakuangakia population growth.

Na kwenye sensa ya nwaka 2022, rais Samia alisema kuwa inabidi watu watumie uzazi wa mpango, kwa sababu serikali inaelemewa kutoa huduma za jamii, kwa sababu watu wanazaana sana.

Maana yake ni kwamba, kuanzia mwaka 1965 mpaka leo, serikali imeshindwa kuongoza vizuri elimu ya uzazi wa mpango.

Zaidi, habari hii inaonekana si kipaumbele. Sera za serikali zipo, lakini kila rais anaamua azifuate, azisahau, au hata azipinge. Tumeona chini ya Magufuki, rais aliamua kuzipinga sera za uzazi wa mpango kwa kusema watu wazae tu, yeye atasomesha.

Tuna tatizo la elimu, lakini pia tuna tatizo la utamaduni. Tunatafuta quantity of life bila kujali quality of life.

Kwa birth rate yetu inayokaribia 4%, nchi ita double population every 22- 23 years or so. Maana yake ni kwamba, kufikia mwaka 2050, miaka 25 kutoka sasa, Tanzania itakuwa na watu milioni 130.

Watu wengi wanasema kuongeza watu ni jambo zuri, tunahitaji nguvukazi zaidi, tunahitaji soko kubwa zaidi. Lakini, ukiwa hujui kuitumia nguvukazi hii tuliyonayo, kuongeza nguvukazi hakukusaidii kitu. Ukiongeza soko la masikini watupu, kuongeza soko hakukusaidii kitu. Sanasana utaongeza migogoro tu ya watu kugombea resources na hata kusababisha vita ya wenyewe kwa wenyewe.

Suluhisho ni nini?

Kuna mengi ya kufanya, lakini kitu kikubwa kabisa ni kuzidisha elimu. Jamii zilizoelimika automatically zinapunguza uzazi. Kwanza kwa kuelewa suala la quality vs. quantity of life wasomi wanakuwa na watoto wachache ambao wana maisha bora. Lakini pia, kuongeza miaka ya watu kusoma elimu rasmi, hususan wanawake, kunapandisha juu umri wa kuanza kuzaa. Na kwa kuwa wanawake wana miaka fulani tu ya kuweza kuzaa, ukipandisha juu umri wa kuanza kuzaa, kwa mfano kutoka miaka 18 mpaka miaka 25, hapo utakuwa umepunguza idadi ya watoto kwa huyo mwanamke.

Lakini pia, wanawake wengi walio wadogo, wasio na elimu, wanazalishwa bila kupenda, bila kupanga. Wanawake walioelimika zaidi, wenye kazi zao nzuri na kipato chao, wana nafasi kubwa ya kupanga pamoja na waume/wanaume zao ukubwa wa famolia na muda gani waanze kuzaa.

Hili jambo litasaidia si tu kupunguza ukuaji wa idadi ya watu, bali pia litasaidia kuweka usawa zaidi kwenye maamuzi ya kuzaa yakae kipamoja zaidi, wanawake wasizalishwe tu bila wao kuwa na maamuzi katika suala hilo.

Kuna mengi ya kufanya, lakini hili la elimu, hususan kwa wanawake, litasaidia sana.

Nchi kama Iran, nchi ambayo ni ya Kiislamu (na hivyo tungetegemea wanaume wawe na sauti kubwa sana na idadi ya watoto kwa kika mwanamke iwe kubwa), imeweza kupunguza sana idadi ya watoto kwa kila mwanamke, kwa muda mfupi, kwa kuwasomesha wanawake wake.

Iran ni mfano mzuri wa kutuonesha kuwa, tukiamua, tunaweza kupunguza birth rate Tanzania.

Back
Top Bottom