Ni wazi mgombea wa upinzani nchini Zambia atatangazwa mshindi.
My concern is: Historia inatukumbusha kuwa Hichilema aliwekwa ndani na Lungu kwa kumpa kesi ya kumbambikia ya Uhaini. Mahakama ikamweka huru.
Kwa akili za Waafrika tulivyolaaniwa, huyu mteule Hichilema atafanya hayo hayo kwa Wapinzani wake Mara akiapishwa.
It is a matter of some few days to come we will witness atrocities commanded by him against opposition as we see Samia "killing" Mbowe!
Mleta mada elewa kuwa duniani kote tawala za binadamu zinaandamwa na hulka za ubinafsi. Ndio asili ya binadamu. Hata nchi kama Marekani (US) inayochukuliwa kama ngome ya demokrasia iko katika mapambano ya kudumu dhidi ya hulka zinazotishia uhai wa demokrasia huko. Mfano mzuri ni jinsi nchi hiyo ilivyokabiliana na uongozi na wafuasi wa aliyekuwa Rais, Donald Trump na vuguvugu lake la MAGA la kutaka kurejesha ukuu wa watu weupe huko US.
US iliasisiwa kwa mapambano yaliyohitimishwa miaka ya 1780 na kazi kubwa ya kuunda katiba makini na kuweka mifumo na taasisi imara zilnazohakikisha nchi haiendeshwi kwa kutegemea hulka za viongozi.
Hivyo usipoteze muda wala kuwa concerned na tabia ya Rais Hichilema huko Zambia. Kuwa concerned na kama Zambia wana katiba makini, mifumo bora na taasisi imara zisizompa Rais absolute power ya kufanya kila ujinga/uovu anaojisikia kuufanya. Kama mfumo ni imara hawezi kufanya huo ujinga unaowaza. Kama sio, lolote lawezekana.
Viongozi wabaya wanapenda sana kuwa na absolute power juu ya mihimili na taasisi zote nchini. Trump alikuwa anamuonea wivu Putin, a strong leader, respected by his people na kumponda Obama. Bahati nzuri, system ya US hailei ujinga.
Afrika tunafanya kosa kubwa sana la kutegemea kupata viongozi “watakatifu” modeli ya masihi, mitume, au malaika. Halafu sisi tuwakabidhi akili zetu watuendeshee nchi kwa “busara na hekima zao”. Yaani tuishi kwa fadhila na huruma zao. Unasikia kauli kama: “ikimpendeza Rais, anaweza kuagiza mshahara uongezwe kwa asilimia ...”
Huko Afrika ya Kusini, ANC walipoingia madarakani 1994, haikuchukua muda viongozi weusi, kwa tamaa zao, wakaanza harakati za ufisadi kwa kasi ya 4G. Ironically, mfumo wa utawala ulioasisiwa na makaburu, ukawafunga breki.
Tuitazame Zambia kwa undani. Hichilema ni mtu binafsi na ubinafsi wake. Sio mtakatifu fulani. Hoja muhimu ni je, nchi inamruhusu kufanya lolote analotaka? Mfano mzuri tunao hapa kwetu - sisi tunaosubiri lini masihi atashuka kuja kututawala.