Waafrika wamelaaniwa: Hichilema utafanya yaleyale ya Lungu ya kuonea Wapinzani

Nimecheka sana hadi mbavu zimeniuma. Eti Rais Lungu ana pinga uchaguzi haukuwa huru na haki free and fair. Kinachonichekesha ni rais aliyopo madarakani incumbent Africa anamlalamikia uchaguzi haukuwa huru na haki. Just imagine Africa. Wazambia wapewe tuzo.
 

Very wrong idea, sorry.

Ukikabidhiwa dhamana kuu ya kuongoza nchi kama Tanzania, kiongozi makini, unatakiwa kuwa na uono (vision) wa mrefu hasa usiopungua miaka 100 mbele kuhusu mustakabali wa taifa.

Unatakiwa uwe JUU ya mitizamo finyu kama jazba na visasi kwa watu duni. Nchi zetu hizi zimejaa wachumia fursa (opportunists) wasiokuwa na msimamo wa maana. Usitake kujionyesha unapambana na hao kama kazi yako kubwa. You have a bigger mission.

Hivyo, sahihisha makosa yaliyo dhahiri, acha taasisi husika zichukue hatua inapobidi kwa mujibu wa utawala wa sheria na tafuta maridhiano panapostahili na penye tija. Na wewe ukianza na kauli kama wabaya wako “watalimia meno, wataishi kama mashetani...”, unakuwa hauna maana tena pengine wa ovyo kuliko uliowabadili madarakani.
 
Huu ni mfano mzuri wa demokrasia, siyo hapa Tz ambapo tume ya uchaguzi inajigeuza kufanya kazi za uenezi za chama.
 

Sawa. Ushindi wa Hichilema nadhani ni dalili nzuri sana kwamba Zambia is on the right track. Halafu umesema mahakama ilimuokoa Hichilema kutokana na kuwekwa jela kwa uonevu. I can’t imagine it happening here.

Inaonyesha conscious ya Zambia katika masuala ya demokrasia na haki za binadamu tayari iko juu. Naona hakuna haja ya kuwa na wasiwasi mwingi kuhusu yeye kugeuza saa na kuirudisha Zambia kwenye udikteta wa ovyo.

Ni bora mkuu uendelee kuwa na concern kuhusu sisi tunakoelekea. Giza bado kubwa sana mbele. Zambia tayari mwanga umeanza kuonekana mwishoni mwa handaki.
 
You are absolutely right! Lakini unaona Lungu ametoa waraka kuwa uchaguzi siyo huru na haki... it sounds bit of danger to me anyway. Suppose ana wa lure wanajeshi, what next? ndio wasiwasi wangu, lkn kama ulivyosema Zambia wako mbele sana na wako tayari kuilind demokrasia yao hata mbele ya vifaru. hapa TZ hapana, tunaogopa hata sindano za chanjo per se!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…