Storywriter
Senior Member
- Jan 8, 2023
- 175
- 389
Watu wenye maarifa, elimu na ufahamu hawapewi kipaumbele sana hapa kwetu. Hawaheshimiwi, wala kuthaminiwa sana. Hii imekuwa moja wapo ya sababu za kurudisha maendeleo nyuma.
Wapo watu waliojitolea maisha yao yote kwa ajili ya kuisaidia jamii, kwa mfano madakatari bingwa wanaotibu magonjwa ya kufisha, wataalamu wa sayansi ya kilimo wanaotengeneza mbegu za kisasa, walimu na wahadhiri wakubwa wanaofanya tafiti za kisomi kwa manufaa ya jamii, wataalamu wa sayansi ya mawasiliano wanaotengeze mifumo ya ki-electroniki kwa ajili ya shughuli za kupeleka habari, kukusanya, kutunza na kusambaza data na taarifa.
Tumewapa kipaumbele sana wapiga porojo. Watu wasio na ufahamu na maarifa ya kutosha namna dunia inavyojiendesha na mifumo yake. Kuna wakati eti hawa wapiga porojo wamekuwa na amri zidi ya watalaamu na mabingwa
Utakuta eti diwani wa kata anayejua kusoma na kuandika tu anamkataa daktari aliyekaa darasani miaka 5. Utasikia "sitaki huyu dakatari afanye kazi kwenye kata yangu". Naishauri Serikali isikubali kabisa upuuzi wa hawa wapiga porojo.
Tukitaka kutoka hapa tulipo kama taifa lazima tuheshimu wataalamu. Tukatae kuendekeza wanasiasa uchwara wasio na tija yoyote zaidi ya majungu na fitina.