mamabaraka
Member
- Oct 18, 2011
- 92
- 14
Hawapendi wangezaliwa Kama sio Hao wanawake? Wanajitoa fahamu mbona wakezao wakiwa na mimba wanafurahi japo mimba si zao...
Hawapendi wangezaliwa Kama sio Hao wanawake? Wanajitoa fahamu mbona wakezao wakiwa na mimba wanafurahi japo mimba si zao...
Hata ofısı za Serıkalı ıkıtokea wanawake wengı wakıpata mımba kwa mfuatano mabosı wa kıume mara nyıngı hawafurahıı kwa sababu kazı zınalala sana hasa wakatı wa maternıty leave. Ingawa sıyo kosa lao kwanı hakuna anayekuwa akıjua kuwa kıpındı hıcho hıcho mwenzake pıa anapewa ujauzıto.
Upande mmoja inauma ila kwa upande mngine ukizingatia sio kosa lao, wenyewe wanatafuta productivity.
Naweza kusema ni kosa la paternalist system nzima, inayo toa value kwa kazi za watu wasio shinda nyumbani kusaidia basic needs za reproduction, feeding, shelter na mengine. wanaume au wanawake wanao taka kuonekana productive leo, lazima wacompete katika field za nje ya zile primary needs, huku ikiwa vigumu kwa mwanamke kuziacha moja kwa moja.
Kama system inge ipa thamani kazi watu wanayo ifanya hata manyumbani kwao kama kazi za ndani, za kulea watoto, kupika na kadhalika, kwa kweli hawange lazimika kutafuta hizo kazi za ofisini ikiwa bado wanataka kua na watoto kila miaka miwili au mitatu.
Ni swala ngumu sana kutatua.
kwa ukweli mabosi wengine hawako wazi kwa akina mama ni vema kuwajali manake nao wana wake zao na watoto nyumbani. tujue watoto ni taifa la kesho, sasa mama akienda matenity leave ndo majungu yanaanza! oooh jamaa hawafwati nyota ya kijani? tena ukute ndo umeunganisha kila mwaka mazee unalooooo!!!!:tongue:
ofisi nyingne inaeleweka kuwa matenity leave inatolewa baada ya miaka mitatu, lakin kwa wanaume mnaochangia mada pia muangalie mkeo anafukuzwa kazi kisa mjamzito. Tena ofisi nyingne washenzi kweli ukigundulika una mimba unapewa barua ya kufuzwa kazi. Kama tatizo ni productivity itaftwe another alternative kuwasaidia kina mama. Kama anapata mimba kila mwaka apewe likizo bila malipo, lakin kama mtu anafata utaratibu inakuwaje kumwachisha kazi? Na saa nyingine mama wa watu ni mchapakazi kweli kweli? Its not fair.

Tatizo sio mke wa nani, tatizo ni nini mwenye kampuni ametarget wakati anaanzisha kampuni yake. Wewe mwenyewe ni mfano wa mtu asiyejua mshahara unatoka wapi. Unaposema fulani apewe likizo bila malipo, kazi za huyo fulani anayepewa likizo bila malipo anazifanya nani? Lets be realistic, the business is about bargaining and not begging. Hakuna kitu kama kuwasaidia kina mama kwenye accounts.
Unashauri waajiri wawe flexible kwenye attendance bila kujali mishahara inatokana na uzalishaji. Your only alternative ni kumpa likizo bila malipo, kwa hiyo aajiriwe mwingine au? Wanawake wawe na shughuli za kufanya. Hata haukuwa mpango wa Mungu kumu- engage mwanamke kwenye direct production na ndio maana tuna complications za namna hii. Unaweza ukaniona mbaya kwa ninayoyasema lkn zingatia uhalisia huu.
Piga hesabu una genge lako la kuuza nyanya na vitunguu. Wakati una mimba, tayari una mtoto mwingine mdogo wa miaka miwili. Kwa wingi wa kazi za nyumbani unashindwa kwenda sokoni kuchukua bidhaa za gengeni, kwa hiyo biashara inaanza kusuasua na baadaye unaamua kuacha kabisa. The same inatokea kwenye makampuni tunayofanya kazi. Kinachotufanya tusione ni kwa sababu sisi hatuko responsible na hasara wala faida ya kampuni, mwisho wa mwezi unapokea mshahara kama umefanya kazi au hujafanya, hilo hujali. Na ndio maana si ajabu ukakuta wanawake wanapiga story huku teller desk za benki zimejaa foleni na hakuna anayejali. Siwalaumu lkn kubalianeni na maumbile na mipango ya Mungu.