Waajiriwa motivation ya kwenda kazini huwa inapungua sana biashara zinapoingiza faida inayolingana na mshahara ndani ya wiki or less, ni basi tu uoga

Waajiriwa motivation ya kwenda kazini huwa inapungua sana biashara zinapoingiza faida inayolingana na mshahara ndani ya wiki or less, ni basi tu uoga

G Tank

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2023
Posts
2,297
Reaction score
8,760
Lets say take home yako baada ya makato yote ni shilingi X per month.

Umeanza biashara yako au umetoka nayo mbali, upepo unavuma wa pesa direction yako yani kila wiki au kwa siku kadhaa chache unafunga hesabu kwa faida ya X.

Kusema kweli hapa ndipo unapoanza kuona ajira ni utumwa hasa zile ambazo hazina ulaji, madili, promotions nzito, n.k.

Unaamka asubuhi kwa kujivuta sana huku unasonya, unawahi kazini ni kwajili ya kusaini, utazuga zuga ukipata kanadfasi tu unachomoka kazi wenye usongo, upo bize na biashara zako.

Uoga wa kuacha ni ule ukoko uliobaki wa saikolojia ya mshahara upo stable kila mwezi, biashara inaweza kuanguka.
 
Na ikianguka kama hukujipanga vizuri hakuna rangi utaacha kuona.

Kuna jamaa aliacha kazi baada ya kuona biashara inakimbiza sana, alidumu nayo miaka miwili tu ilivyofika kipindi ya covid upepo ulivyochange ukaathiri na biashara ikayumba mpaka ikafa.
 
Uoga wa kuacha ni ule ukoko uliobaki wa saikolojia ya mshahara upo stable kila mwezi, biashara inaweza kuanguka.
na sio saikolojia, ndio hali halisi. Zipo biashara nyingi zilizoanguka hadi kufikia kiasi cha kumfanya mfanyabiashara atamani kuajiriwa.

Kwa hiyo hilo nalo uliangalie, usilinganishe tu faida na take home, ulinganishe pia hasara na take home, halafu ufanye projection
 
Back
Top Bottom