Waajiriwa Tz wanakatwa kodi kubwa kuliko wote EAC

M-mbabe

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2009
Posts
13,203
Reaction score
23,027
kutokana na ripoti iliyotolewa na PricewaterhouseCoopers (PWC) hivi karibuni, waajiriwa chini Tanzania wanakatwa kodi kubwa sana ukilinganisha na nchi zote zilizomo kwenye EAC. kama hilo halitoshi, kiwango hicho kiko above world average.

angalia hapa chini....

Tanzania - 18%
Uganda - 11.3%
Burundi - 10.2%
Kenya - 6.8%
Rwanda - 5.6%
World average - 16.3%

another darker side of the Tz taxation system ni kuwa waajiri (mabepari) wanakatwa kodi mdogo kuliko nchi zote ndani ya EAC.

check hapa chini:

Tanzania - 20.4%
Rwanda - 21.9%
Uganda - 25.2%
Kenya - 28.2%
Burundi - 38.6%

mimi ni mhandisi hivyo ukiniambia nianze kutoa tafsiri ya hizi statistics in the context of the micro/macro impacts on our economy ni sawa na kuanza kuniambia niandike kichina!

hata hivyo, kwa tafsiri ya ki-layman tu, je hapa hatuwezi kweli kupata one of the answers za kumpa kama desa mkuu JK kuhusu chanzo cha umasikini wa Watanzania??

wajuzi, naomba mtudadavulie tafadhali..
 
mke wangu katika basic salary ya sh 1,500,000 kodi anakatwa sh 300,000
 
Nchi yetu kutokana na uvivu wa kukusanya kodi na ukweli kuwa kodi za wafanyakazi hazitoi mwanya wa "mazungumzo" ndio maana tunatolewa kafara kufidia hata kodi za wengine.
 

mkuu tunakomaje?yaani sisi ndio mbuzi wa kafara
 
... mbaya zaidi Wafanyabiashara hawalipi Kodi Stahiki na hivyo kumbebesha Mfanyakazi mzigo wote wa Kodi. Wameguswa kidogo tu kwenye matumizi ya EFD, utafikiri wamepigwa chamoto makalioni na sie Wafanyakazi tumeunga mkono!
 
Nchi yetu kutokana na uvivu wa kukusanya kodi na ukweli kuwa kodi za wafanyakazi hazitoi mwanya wa "mazungumzo" ndio maana tunatolewa kafara kufidia hata kodi za wengine.

1. tax base is very narrow...embu angalia kiwango cha informal sector (machinga kila kona, etc)

2. corruption....I believe that grand corruption ndicho chanzo kikubwa cha low corporate tax wanayolipa hawa mabepari.
 
... mbaya zaidi Wafanyabiashara hawalipi Kodi Stahiki na hivyo kumbebesha Mfanyakazi mzigo wote wa Kodi. Wameguswa kidogo tu kwenye matumizi ya EFD, utafikiri wamepigwa chamoto makalioni na sie Wafanyakazi tumeunga mkono!


Sasa wewe unaongea nini hapa??????!!!!!

Kama tunaumia sisi waajiriwa haina sababu ya kusema ya wafanyabiashara,wao hawana nidhamu ya woga ndio maana wamegoma mchana kweupe.!!!!!!!

Huku kwenye ajira unafiki mwingi sana ndio maana hakuna umoja wa kweli na ukweli ni kuwa watu utendaji uko chini,commitment ,upigaji wa miradi,safari hewa na kizushi ndio usiseme kabisaaa ndio maana moral authority ya kusimama na kusema hatuna!!!!
 
shkamoo mzururaji,
nisamehe mimi mwenye elimu ndogo ya kutokuelewa maana ya source/reference ama acknowledge,
naomba kujuzwa maana akisema source ------ yangu ndo naweza kujua ( kwa mujibu wa mzururaji)
Report ya mwaka gani, inapatikana wapi? Maktaba, mtandaoni ama jarida lipi ili tuipitie ! si kila chanzo ni chanzo, na si kila chanzo kipo, na si kila chanzo kilichopo ni chanzo reliable, na si kila chanzo reliable kipo accessible! and many more.....
Nawapongeza wenzetu wasomi wa vyeti, maana tukiuliza tutaambiwa una Masters ama phd of that kind!
 
Hii nchi aisee tunanyonywa sana hadi inauma
 
1. tax base is very narrow...embu angalia kiwango cha informal sector (machinga kila kona, etc)

2. corruption....I believe that grand corruption ndicho chanzo kikubwa cha low corporate tax wanayolipa hawa mabepari.

Haswaaa....!
 
Yaani mimi nilimsikia waziri wa madini na nishati akisema serikali inapata 2% kutokana na mauzo ya madini. Kusema ukweli takwimu hiyo imenipa shida sana kuelewa. Ina maana makampuni ya madini yanasepa na 98% halafu mtu aseme madini ni yetu watanzania? Sio yetu tunawatunzia wenye nayo.
 
it's good kuona jana wabunge wakiliongelea hili suala la kodi kwa waajiriwa vs waajiri.

we need some urgent action kutoka kwa serikali kuhusu hili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…