The problem solutionist
Member
- Jan 28, 2024
- 17
- 10
Kumekuwa na tatizo la ukosefu wa uwajibikaji na uwajibishwaji wa viongozi wa hospitali ya Manispaa ya Kahama mjini kwani kero ni nyingi wanazokumbana nazo wafanyakazi ikiwemo waajiriwa wapya wa mwaka 2021 pesa zao ambazo walipaswa kulipwa haki yao hawakupewa lakini kwenye salary sleep zao zinaonesha kuwa walilipwa na wapo wengi lakini wakienda benki kuomba statement pesa hazionekani lakini toka mwaka huo mpaka leo hawajalipwa pesa zao lakini kwasababu kumekuwa na mazingira ya vitisho wanaogopa kusema hivyo.
Tunaomba viongozi wa juu wanaohusika wafuatilie hili suala pesa za watumishi wapya hawa kwanini hawajalipwa na anayehusika kwanini hajachukuliwa hatua mpaka leo?
Je, kwa hali hii rushwa tutaweza kuidhibiti?
Tunaomba msaada ili watumishi hawa wapate stahiki zao na haki itendeke. Wanafanya kazi kubwa mnoo ya kuwahudumia wagonjwa na sio wao tu, nchi nzima wauguzi na madaktari wanafanya kazi kubwa lakini hakuna motisha.
Nina imani Serikali inafanya kazi yake kwa sehemu yake ipasavyo shida ni viongozi waliokasimiwa madaraka wanayatumia vibaya.