Waalimu mlirudi kazini kweli au ni abrakadabra?

MotoYaMbongo

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2008
Posts
2,146
Reaction score
886
Waalimu ndg zangu nawauliza ni kweli mlirudi kazini au abrakadabra na mazingaombwe mlioyafanya? Kwanza kabisa nauliza hivi kwa sababu sioni kabisa dalili za nyie kuwepo kazini kwani picha halisi tumeziona kwenye matokeo ya mitihani ya watoto wetu wa drs la saba japo serkali na yenyewe imecheza filamu ya namna yake kwamba ufaulu umeongezeka kwa asilimia 8.8 na wakati wamechagua wanafunzi waliopata alama chini ya nusu yaani alama 60 kati ya 250 huu si usanii na usaliti wa taifa letu?Sasa sijui serkali ina malengo gani na Watanzania? Sasa hapa nauliza wazazi ambao ni wananchi pia mna malengo gani na watoto pamoja serkali hii inayotupa dira ya namna hii, kwa waalimu wao walisharidhika na wanachokipata lakini je mko kazini kweli au ni mazingaombwe
 
Mkuu hali halisi ya maisha hasa ya hao unaowaita Waalimu unayajua, jitahidi basi kuwaombea kwa mkuu wa kaya awajali japo kidogo. Hata kwa kuwapa matumaini tu, maana ule mgomo uliopigwa BAN na mahakama na kuwaambia wawalipe fidia wanafunzi labda ndo hiyo!!?? Jamani kama hatujaamka sisi wazazi hili bomu ni letu, litatulipukia wote. Hao waliochaguliwa ndio watakuwa viongozi kuanzia ktk kaya hadi taifa, wataalamu wetu ktk vitengo mbalimbali mnategemea nin? Pia kuna kundi la hao waliomaliza K4 mwaka 2009, 2010, 2011 na tunaowasubiri(matokeo yao) wa 2012 haya nayo yasemekana ni mabaya mno labda wachakachue. Sisi wazazi tuamke kabla jogoo hajawika tusiitegemee serikali maana watoto wa viongozi wapo hukooo....wapi kule, ah! Eehee...kule Saint naniliu kule wanapewa elimu ya kweli sisi wa kwetu wanabaki kung'aa macho tu. Kalaghabaho.
 

watanzania jamani kwa kulalamika! mkuu mbona hiyo picha ndo kwaanza inaanza! sasa wewe tayari ushaanza kulalamika mbona kitu bado kabisa! hii kitu hadi Serikali iache 'polly tricks'
 

Umenena haswaaaa! Wakati mwingine najiuliza hivi wazazi wetu kweli wapo? Na ingelikuwa vyema tungelikuwa na umoja wa Wazazi nchi hii iwe na uwezo wa kukosoa, kukemea na kushauri vijana na hata serikali kwa ujumla wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…