Tetesi: Waalimu sasa kuanza kupigwa picha pindi wanapoingia darasani

BRAND

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2013
Posts
296
Reaction score
257
Katika kuhakikisha kuwa walimu wanaingia darasani kumeandaliwa utaratibu wa kuwapa tablet walimu wakuu na wakuu wa shule ili kumpiga picha kila mwalimu pindi anapoingia darasani ili kuthibitisha kuwa amefundisha!

Mara baada ya mwalimu kupigwa picha itatumwa kwenye ofisi za elimu wilaya ili
kuthibitisha kuwa mwalimu fulani ameingia darasani na amefundisha!
Hii taarifa ni kwa mujibu wa rafiki yangu wa karibu mwalimu wa primary mojawapo iliyopo wilayani kongwa dodoma ambapo tayari wao wameshapewa taarifa rasmi kupitia mwalimu mkuu wao kwamba utaratibu huo utaanza hivi karibu hivyo wajiandae kwa hilo!
 
Kwani hamna daftari la walimu la ku sign kila pindi mwalimu wa somo husika kumaliza kipindi chake?

Vitu vingine bhana!
 
Posho ya laki 2.5 ndiyo wanayopewa wakuu wa shule na walimu wakuu tangu august nje ya mshamshahara kwaajiri ya shughuli za kiutawala
 
[emoji121]
WEKA PICHA YA UTHIBITISHO TAFADHALI MKUU!
 
Posho ya laki 2.5 ndiyo wanayopewa wakuu wa shule na walimu wakuu tangu august nje ya mshamshahara kwaajiri ya shughuli za kiutawala
sio kwa ajili ya utawala ni hela yao kabisaaaa, hela ya utawala si ipo kwenye zile za magufuli za elim bure
 
Kwani hamna daftari la walimu la ku sign kila pindi mwalimu wa somo husika kumaliza kipindi chake?

Vitu vingine bhana!
Kusaini kwenye register/attendance book kunaweza fogiwa, lakini alama za vidole/picha/sauti ni uthibitisho pasipo shaka.

Katika hili tulichelewa Sana kwani kutumiaTehama katika kukuza Uchumi na ustawi wa jamii ni jambo muhimu.
 
Hii kitu ni non sense hizo tablet zipo ngapi! na je atawezaje kupiga picha walimu wote watakaokua na kipindi muda huo au ndo wengine watasitisha ma pindi yao mpaka apigwe picha kwanza ni bora nguvu iwekezwe ki namna nyingine kuboresha elimu yetu ya hapa tz sio kutuletea maigizo kama haya
 
Hapo hakuna walichofanya..!
Labda wachukue video lakini si picha inayopigwa chin yadakika
 
Watapiga hadi picha za uchi sasa!. Too much, mm siwezi kubali ujinga kama huo. Ndio maana nilijikimbizaga mapema na tubarua twao twa kujiunga kusomea teaching!
 
Back
Top Bottom