Waalimu sasa wazinduka!

Joined
Jul 12, 2013
Posts
6
Reaction score
2
"Wanasema kweli kikulacho kinguoni mwako" baada ya kunyonywa kwa mda mrefu na CWT waalimu waanzisha harakati za kujikomboa nchi nzima kwa wewe usienataarifa hebu pitia muhtasali wa barua kamainavyoeleza hapo chini;



KAMATI YA WANACHAMA WA CHAMA CHA WALIMU TANZANIA YA KUDAI HAKI NDANI YA CHAMA

S.L.P 90226
SIMU 0756 941000 / 0783 754112 DAR ES SALAAM,

KUWHT/CWT/5/1 04/07/2013 Msajili wa Vyama vya Wafanyakazi na Waajiri Tanzania, S.L.P 9014, Dar es salaam.
YAH: MAOMBI YA KUSIMAMISHA SHUGHULI ZOTE ZA CHAMA CH WALIMU TANZANIA KWA UKIUKWAJI WA MASHARTI YA USAJILI KWA MUJIBU WA SHERIA NA 6/2004.
UTANGULIZI:- Sisi ni wanachama wa CWT ambao tumeunda kamati kwa ajili ya kukosoa mambo ambayo kimsingi yanatendwa na kukiukwa na viongozi wa Chama cha Walimu Tanzania. Tunakuhakikishia kuwa kamati hii inafahamika vizuri ndani ya chama cha Walimu Tanzania, hasa ikizingatia kuwa tayari tumewahi kukaa na uongozi wa C.W.T na kujadiliana nao mambo kadhaa yanayokiukwa katika utendaji kazi wa CWT. Lengo letu la hapo awali, lilikuwa ni kuwataka viongozi wa CWT kuheshimu masharti ya usajili wa Chama cha Walimu, kama sheria ya AJIRA NA MAHUSIANO KAZINI NA. 6/2004 inavyoelekeza baada ya kutambua na kuridhika kuwa uongozi wa CWT unakaidi kuheshimu LENGO kuu la uendeshaji wa shughuli za kichama kwa mujibu wa sheria za nchi, sisi wanachama na walimu tumeamua kuleta kwako maombi juu kuzuia CWT isiendelee kufanya shughuli yoyote ndani ya Jamhuri ya Muungo wa Tanzania. Mambo yanayoleta utata na hatimae kupelekea sisi kuleta maombi haya kwako ni pamoja na:-
  1. Katiba mbovu,
  2. CWT kujihusisha na biashara
  3. Kutotetea wanachama walimu
  4. Kutofuata katiba
  5. Faida itokanayo na vitega Uchumi kufujwa,
  6. Viongozi wa CWT kutotoa taarifa ya mapato na matumizi ya Chama kwa Wanachama na walimu.
  7. Uundwaji wa Kampuni ndani ya chama (Inayojulikana kama TDCL.)
Tunaomba kutoa maelezo yetu kama ifuatavyo: Ili uweze kuchukua hatua za kuzuia shughuli zote za CWT, ambazo sisi tunaamini zinafanywa kwa ukiukwaji wa sheria, na kukosa maadili ya vyama vya wafanyakazi. 1. UBOVU WA KATIBA YA CWT. Sisi kundi tunaamini kuwa, katiba inayotumika hivi sasa na CWT haifai kwa sababu katiba hiyo Toleo la Tano la mwaka 2009 ambayo ilirekebishwa tarehe 18/12/2009 inayo mapungufu ambayo kimsingi hayawezi kuvumilika. (i) Katiba inaruhusu kufanya Biashara. Katiba hii ya CWT imepitishwa katika Ofisi yako kuwa ni Katiba halali ya CWT, lakini sisi tunaona waziwazi kuwa, Katiba hii ya CWT inakiuka sheria namba 6/2004 - KIFUNGU CHA 46 (i) juu ya masharti ya usajili wa chama. Kifungu hiki kinaweka masharti ya kusajiliwa kama chama cha wafanyakazi (b) Jumuiya isiyo na lengo la kujipatia kipato. - KIFUNGU CHA 47 (I) (b) juu ya masharti ya kikatiba. Kifungu hiki kinaweka bayana kuwa Katiba na kanuni za chama cha wafanyakazi, jumuiya ya waajiri au shirikisho:- (a) Itaeleza kwamba ni chama ambacho hakipo kwa ajili ya kutafuta kipato Ukisoma katiba ya CWT ambayo imesajiliwa na ofisi yako inaweka wazi juu ya kufanya Biashara, jambo ambalo ni kinyume na vifungu vya 46 na 47 vya sheria ya AJIRA NA UHUSIANO KAZINI NA. 6/2004. Tukiweka wazi biashara zinazofanywa na CWT ni pamoja na kukusanya kodi kubwa, kutoka jengo la MWALIMU HOUSE, kodi inayolipwa na wapangaji. Pia CWT imeanzisha Kampuni ndani ya chama, kampuni inayojulikana kama TDCL na pia CWT wako katika hatua za mwisho kuanzisha Bank. Mara baada yakuona jinsi ambavyo CWT inaendeshwa kinyume na masharti ya usajili wake na pia kinyume na maadili ya Vyama vya Wafanyakazi, wakati huo huo, ofisi yako inawatambua, sisi tunaomba ufafanuzi kutoka ofisini kwako, yawezekana ikawa ni Elimu kwetu hatukuielewa vizuri Sheria Na. 6/2004 kama inavyoweka masharti ya kusajiliwa chama cha Wafanyakazi (Rejea katiba ya CWT kifungu cha 4 (s) toleo la tano – 2009) 2. KATIBA KUFUTA MATAWI MAHALI PA KAZI Kwa makusudi kabisa imefuta uwepo wa Matawi mahali pa kazi kupitia Katiba hiyo toleo la tano la mwaka 2009. Na Katiba hii kuonyesha kuwa uwakilishi wa Wanachama ni wa mwakilishi mmoja mmoja kutoka katika shule au vyuo au Taasisi, jambo hili ni kinyume na taratibu za uundwaji wa Vyama vya Wafanyakazi, kwani katika chama cha wafanyakazi, lazima kuwe na uwakilishi pale ambapo kuna wafanyakazi zaidi ya 5 kwa kuunda tawi, tawi ambalo litakaa na wafanyakazi ambao ni wanachama kwa ajili ya kutoa maoni yao na pia hata katika kuunda mabaraza ya wafanyakazi mahali pa kazi, ni lazima kwanza tawi la chama cha wafanyakazi liwepo kwa ajili ya kutoa wawakilishi. Pia tawi linafanya kazi ya kujadiliana na mwajili kuhusu mambo mbalimbali ya wanachama kulingana na mazingira ya kazi ya mahali pa kazi. Katiba ya CWT imefuta matawi kupitia vikao vya CWT bila kupata maoni ya wanachama juu ya jambo hili, tunafahamu kuwa matawi ndio yanayoiunda Wilaya na Wilaya inaunda Mkoa, sasa iweje vikao vya CWT vianzie ngazi ya Wilaya na hali wanachama wa CWT wapo chini ya Wilaya ambako ndiko matawi yanatakiwa kuundwa, tumeshangaa Katiba ya aina hii kupata usajili katika ofisi yako. 3. UUNDWAJI WA KAMPUNI NA KUANZISHA BENKI NDANI YA CWT. CWT imeunda Kampuni inayoitwa TDCL, lengo la Kampuni hii ni kwa ajili ya kutafuta kipato zaidi ndani ya chama cha Walimu, na pia CWT wako hatua za mwisho kuanzisha BENKI, ambayo pia lengo kuu ni kupata kipato zaidi kutokana na faida itakayopatikana kwa taratibu za kibenki. Ni jambo la hatari kuona kwa makusudi viongozi wa ngaizi za juu wa CWT, wanafanya vitendo ambayvo vinakiuka Sheria Na. 6/2004 na hata kupata baraka za msajili wa Vyama vya Wafanyakazi Tanzania. Mapato yanayotokana na uwekezaji wa vitega uchumi ndani ya CWT havina tija kwa wanachama (Walimu) kwani fedha hizo hazina manufaa hasa pale ambapo hazionekani zinapokwenda. Tunakuomba usitishe kabisa Shughuli za CWT, kwani hivi sasa sio chama cha Walimu tena. Ukitazama kwa makini vifungu vingi ndani ya Katiba ya CWT utaona kuwa wanatumia sana Jina la Mwalimu mahali ambapo wanapaswa kumtaja Mwalimu kama Mwanachama mfanyakazi. Hii ni dhahiri kuwa CWT ipo kwa ajili tu ya chama cha KITAALUMA na sio vinginevyo, na ndio maana viongozi wanafanya mambo ambayo hayakidhi maadili ya vyama vya wafanyakazi ambavyo lengo kuu ni kuinua hali za wafanyakazi. 4. CWT KUTOWEKA WAZI TAARIFA YA MAPATO NA MATUMIZI KWA WANACHAMA WAKE. Ni wazi kuwa chama cha wafanyakazi kilichosajiliwa ni lazima kitoe taarifa za mapato na matumizi katika Daftari ambalo kila Mwanachama anaweza kufanya ukaguzi ili kuona kama mwenendo wa chama katika masuala ya fedha zinazotokana na ada au michango ya wafadhili, zinatumika vizuri. Hii ni kwa mujibu wa Sheria Na. 6/2004 Kifungu cha 51 (2), kifungu hiki kinaweka wazi kwamba, taarifa za fedha za ripoti ya mkaguzi itawekwa wazi katika ofisi za chama ili wanachama waweze kuona. Hakuna siku hata moja ambayo CWT imewahi kutekeleza Sheria hii. Jambo ambalo tunaona kuwa CWT haistahili kupewa hadhi ya kuitwa chama cha wafanyakazi. Hii ni kutokana na aina ya mwenendo ambao chama hiki kinafanya kwa faida ya viongozi wa ngazi za juu, ambao yawezekana kwa sasa ni matajiri wakubwa na hivyo wanaona ni sahihi kubadili CWT kuwa Kampuni. Katika mchakato huu wa kuanzisha Benki, je walimu ambao hawatanunua hisa, watanufaika vipi? Wakati Benk imeanzishwa na pesa za vitegauchumi ambavyo amevichangia? Hakuna maelezo ambao kwa wale walimu ambao hawatanunua hisa, sasa watanufaika vipi? 5. KUANZISHWA KWA WANACHAMA WANAWAKE NDANI YA CWT Tumegundua jambo kubwa ambalo ni ukiukwaji wa muundo wa CWT. Viongozi wa CWT ngazi ya Taifa wamelazimisha kuweka utaratibu, wa kuwa na kitengo cha uwakilishi wa wanawake. Huu ni upotokaji wa misingi ya vyama vya wafanyakazi, kwani wafanyakazi wote wanaunguanishwa na Sheria moja ya AJIRA NA MAHUSIANO KAZINI NA 6/2004 kifungu cha 4 katika tafsiri ya mwajiriwa. Na waajiriwa wote katika kuunda chama cha wafanyakazi ni kutafuta mshikamano wa pamoja Sasa ni vipi tena ndani ya chama cha wafanyakazi kuanzisha Kitengo cha Wanawake ‘eti’ kinachotetea haki za wanawake katika uwakilishi, kama ni hivyo wanawake ambao ni waajiriwa wanaweza kuunda umoja wao wa kutetea mambo yao nje na mfumo wa CWT. Hivyo sisi tunaona kuwa utaratibu huu pia sio mzuri na hivyo tunaomba ufafanuzi mzuri wakati huu ofisi yako ikiendelea na utaratibu wa kuzuia CWT kuendelea na shughuli zake batili vinginevyo wanaume nao waunde kitengo chao. Kuanzishwa kitengo cha wanawake ndani ya chama kunapelekea kuwepo kwa rushwa wakati wa uchaguzi. 6. ATHARI ZA MGOMO Hakuna taarifa kwa wanachama walioathirika na mgomo na hatua zilizochukuliwa, na pia kuna wengine hawajapata huduma stahili kama wanachama kwa kuwa wameathirika na migomo ya CWT. 7. Tunaomba mamlaka husika ziagize viongozi wa CWT wayawekee magari utambulisho na sheria za matumizi ya magari hayo, kwani kwa sasa yanatumika kama mali binafsi. 8. MAONI YA JUMLA Tunakuomba ukizuie chama hiki kwa sababu kimepoteza mweleko wa madhumuni yake ya kutetea haki ya wafanyakazi wake na badala yake wanaelekeza nguvu hizo kwenye biashara ambazo wanachama hawana faida nazo. Ili walimu wafanyakazi wapate kuunda chama chao ambacho kitatii na kufuata maadili ya vyama vya wafanyakazi nchini na Duniani kote, kwani lengo kuu la chama cha walimu ni kutetea haki na maslahi ya wafanyakazi na siyo kufanya biashara kama inavyokatazwa na Sheria ya AJIRA NA MAHUSIANO KAZINI NA. 6/2004 Tunaambatanisha barua KUMB NA. KWW/TIK/DSM/112/ ya tarehe 1/5/2012. pamoja na Muhtasari wa tarehe 27/6/2012 wa kikao cha pamoja na Uongozi wa CWT. Tunawasilisha.
Mohamed Ally
Kny: Katibu
Kamati ya Wanachama wa CWT ya Kudai Haki Ndani ya CWT
Nakala:
  1. Waziri Mkuu - Kwa taarifa na kusaidia walimu kutatua mgororo na chama
chao
  1. Waziri,
TAMISEMI
  1. Waziri
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
  1. Waziri
Wizara ya Kazi
  1. Waziri
Wizara ya Utumishi
  1. Mwanasheria Mkuu

  1. C.A.G

  1. TUCTA

  1. Maafisa Elimu S/M na Sekondari
Tanzania
  1. Wanachama wa CWT (Walimu)
Msingi, Secondary, Vyuo na Taasisi za Elimu
  1. TAKUKURU - Tunaomba ufanye Uchunguzi wa pesa zinazotumika
Makao Makuu
  1. CWT – Taifa

  1. Vyombo vya Habari
Tanzania
MAWASILIANO:0715-941000. M/KITI WA KAMATI (TZ) "ZINDUKA NA WEWE MFAHIMISHE NA MWEZIO"

 
Tunashukuru kwa taarifa Mungu akujalie. Vip kama unajua viwango vipya vya mishara ya walimu especialy hawa wanaoanza kazi,msaada tafadhali!
 
Tunashukuru kwa taarifa Mungu akujalie. Vip kama unajua viwango vipya vya mishara ya walimu especialy hawa wanaoanza kazi,msaada tafadhali!

hahahaha ranya umenichekesha sana, mkuu umekua mpole mbona? nilijua utaanza kuhoji, kuna maswali mengi sana ktk cwt

kwamba hata walisitisha shughuli za chama hayo mafungu ya miaka yote yako wapi? makato yenu, na kodi na miradi mapato yako wapi?
 
Msije mkatekwa kisha kung'olewa meno na kucha
 
tehteh mbona tuliona katibu mkuu wenu sijui anaitwa oliochi akipondaponda TV kwamba nyie hamjui kitu sasa mmesubutuje. ila kama ni kweli mnayoyasema kazeni buti na ilkibidi mwapereke mahakamani kama mnahushahidi mana wao wamezoea kupeleka serekari mahakamani ili kuficha uovu wao, sasa kazi kwao. kila raheri walimu katika jitihada za kujikomboa mungu awasaidie
 
Toka kwenye hiyo Tasnia ya Elimu......utakufa bureeee!
 
Washakula na wanaendelea kula binafsi sina tatizo na Cwt kwan hata wasipokuwepo sioni jinsi mwalimu anavyofaidi jiungeni kwa umoja wenyu muishinikize serikali iongeze mishahara minono na stahiki nyengine
 
Na warudishe matawi mashuleni ili mimi nikiwa pale Benjamini Mkapa Secondary nijue tuna tawi la CWT na si kuna anaejiita eti Rais wa CWT. Waliua matawi kwa ubadhilifu chama gani kinaanzia mkoani. Uliouchi na Mikoba wezi sana wale.
 

Uliouchi janga kwa walimu jamaa anawaona walimu vilaza balaaa...
 
Ahsante sana. Tena CWT hata kuisikia sitaki kabisa ikafie mbali huko. 2% za kila mwalimu yatosha!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…