Waalimu wengi wa sekondari za serikali wana ajira zaidi ya moja

Researcher

Senior Member
Joined
Dec 15, 2010
Posts
187
Reaction score
48
Pamoja na kwamba haujakuwepo utafiti wa kina katika hili, nimejiridhisha kwamba hili limeanza kuwa tatizo sugu na kuna sababu ya kuliangalia swala hili kwa kina ili kunusuru elimu yetu.

Pengine kutokana na ufinyu wa kipato na mfumo duni wa ukaguzi, waalimu wengi haswa wale ambao ni degree holders wamekuwa wakishika ajira zaidi ya moja. Wakuu wa shule za serikali wanatambua na wanawapa ushirikiano walimu wao katika kushiriki utoro huu ambao unadhoofisha ubora wa elimu yetu. Mfumo wa ruhusa za kiofisi pamoja na uhamisho nao ni mgumu kiasi cha kuwafanya walimu wengine kujisomea kozi za full time bila kuwa na likizo na pia kufanya kuishi mbali na shule wanazofundisha.

Napendekeza swala hili liangaliwe na ikiwezekana serikali iboreshe maslahi ya walimu sambamba na kudhibiti uwajibikaji wao.

Nasisitiza tena kwamba wapo walimu wengi sana wenye ajira zaidi ya moja na swala hili lisipochukuliwa hatua tutazidi kuudidimiza mfumo wa elimu Tanzania!
 
Nenda kafanye utafiti wako halafu ukimaliza urudi maana naona hapa bado hujafanya hivyo Elimu inashuka kwa kuwa mwalimu na elimu kwa ujumla havipewi thamani yake mbele ya jamii cha kufanya ni kitu kidogo kuboresha maslahi na mkuboresha miundombinu
 
Inawezekana kuna ukweli lkn ni kwa waalimu wa mijini tu maana vijijini hiyo ajira nyingine inatoka wapi? Kuna umuhimu wa kuboresha maslahi yao ili kupunguza utoro maana waalimu wengi sana wana mikopo na mishahara kwa sasa inachelewa mno kutoka hivyo baadhi yao wanashindwa kufika shuleni kwa kukosa nauri hasa wa mijini.
 
harakat Mkuu naona umemjibu mleta mada, maana naona anajichanganya tu wakati kila kitu kiko wazi
 
ilo lipo wazi kabisa kutokana na kipato kidogo xo inawabidi nao watafute kazi za ziada, na pia kumbuka kuwa walimu nao wanafamilia zinazohitaji matunzo kama walivyo watoto wa mawaziri, wabunge, wakuu wa wilaya na wengine, so unambidi kwani kipato chao ni kidogo na ndiomaana wanatafuta namna nyingine ya kuishi. Na ndo utakuwa mtindo huo kama serikali haitaangalia mishahara ya walimu kwa jicho la pekee
 
Wewe mleta mada utafiti wako unaonesha wana ajira mbili,ipi na ipi? Maana kama ni ktk nyanja ya elimu,kwani tatizo liko wapi?Kwa mfano,mwalimu wa hesabu au sayansi akifundisha shule hata kumi,tatizo liko wapi?

Halafu vipi mtu mmoja akiwa mbunge wakati huo huo ni mkuu wa mkoa na mwenyekiti wa bodi ya pamba au kahawa,je huyu yeye ana haki zaidi ya mwalimu? Au labda mimi ndio sijaelewa unachotaka kutufahamisha mkuu?
 
kwani ni dhambi kufanya kazi zaidi ya shule moja? Tuache majungu, mimi ni mwalimu nasubiri ajira ila tayari nafanya tempo shule mbili sa nikiajiriwa itakuwa zaidi
 
Unaweza kuwa mwajiriwa hata wa shule nne,kinachotakiwa ni uwajibikaji kwa mwajiri wako wa kwanza ambako una ajira ya kudumu.Kama unashindwa kuwajibika kwa mwajiri wako basi hauna tofauti na majangiri au mafisadi tunaowazungumzia humu JF kila wakati.Jitafiti ili uje kama unamuibia mwajiri wako muda wake au lah.Kuliko kuwakosesha masomo wasiona hatia basi acha kazi serikalini uhamie kwenye shule binafsi zinazotoa mafao mazuri.
 
Mtoa MADA umekurupuka!, Wewe ume0ma walimu peke?, umewai kuona wapi mchafu akamwambia mchafu mwenzake mchafu?.
Mimi naona hakuna ubaya kama m2 atatimiza majukumu yake.
 
Hivi wewe ndo unaona leo? Unakuwa kama Mwiguli Nchemba wakati akichangia maoni ya kambi rasmi ya upinzani wizara ya Elimu aliyesema eti kusema walimu wanafanya biashara ili kuongeza kipato ni kuwadhaliisha walimu kwani sio wote wanaofanya hivyo, kwa maana nyingini eti walimu hawafanyi biashara ndogondogo ili kuongeza kipato chao, huyu ndiye leo kasema eti ni PHD candindate! Kimsingi hilo swala lipo wazi cha msingi leo tujadili nini kifanyike japo mengi tumeyajadili sema tu hii ni serikali isiyo sikivu!
 
We unajua 2 hzo mbili? Wengne had 4 unaongea 2 na acadmic akupangie ratba ya masomo muda mzur. Btw inahuu.! Hata km wana ajira zaid ya 1 inakuhusu? Km inahusu waongeze mshahara au waje kula kwako.
 

Wapi umeona neno mbili?
 
Mtoa MADA umekurupuka!, Wewe ume0ma walimu peke?, umewai kuona wapi mchafu akamwambia mchafu mwenzake mchafu?.
Mimi naona hakuna ubaya kama m2 atatimiza majukumu yake.

Mimi mada yangu imegusa walimu na sekta ya elimu..wengine wana uhuru wa kuchangia juu ya mawaziri, wajumbe wa bodi na wengine wengi. Kuwepo matatizo katika sekta nyingine hakulifanyi hili lisiwe tatizo.

Unauzungumzia wajibu wa kufundisha shule tatu binafsi au kuwapa elimu bora vijana wa sekondari ya umma kwa mujibu wa mkataba ambao mwalimu binafsi ameuridhia kama full time employee?

Je ni kweli kwamba kwa mujibu wa kanuni na maadili ya utumishi wa uma ukishatimiza wajibu hata kama ni kwa kuwepo masaa mawili kazini una uhuru wa kuwa na mikataba mingine ya ajira na kuitumikia?
 
kwani ni dhambi kufanya kazi zaidi ya shule moja? Tuache majungu, mimi ni mwalimu nasubiri ajira ila tayari nafanya tempo shule mbili sa nikiajiriwa itakuwa zaidi

Shule binafsi hujipanga kupata watakacho toka kwa wanaoingia mikataba nao. Na wasipofundisha wanajua kitakachofuata toka kwa wateja wao. Mimi sizungumzii shule binafsi. Kama una mikataba na shule kumi tofauti za binafsi na una uwezo wa kuzihudumia huo ni ujasiriamali. Ila serikali huajiri waalimu kama watumishi wa kudumu na watumie muda wao wa kazi na juhudi zao zote kama watumishi wa uma. Si kwamba waingie madarasani masaa nane kwa siku lakini yapo majukumu mengine kama kuandaa lesson plan na scheme of work ambayo wanapaswa kuyafanya...
 
Msomage basi kwanza kabla ya kupost.kama wewe inaonekana umeurukia thread na kupost tu bila kuelewa, mimi sijatamka neno mbili popote katika post yangu. Zaidi ya hivyo nimezungumzia swala la kuboreshwa maslahi ya walimu na hiyo si kwa mshahara peke yake..
 


hongera kwa kuliona hilo......
Kaka ukweli ni kwamba hapa tz kilichobaki ni kusema uongo tuuuuu..... Ukisema ukweli kama ulivyosema hapo juu anashambuliwa. Mtu akiibua rushwa anaitwa mnafiki, tukihoji kwanini walimu wachukuliwe wenye alama za chini tunashambuliwa. Unadhani nin kitatokea.... Ualimu kwa leseni, kwa walimu, watatakiwa kua - update kila baada ya miezi sita. Hawajajua nini maana ya hii kitu....wengi watabaki majumbani subiria tuuuu
 
Wapi umeona neno mbili?

Mkuu wangu Researcher huna haja ya kupanic,kwa kuwa wachangiaji wengi wameonekana kuwa kinyume na matarajio yako;hiyo ndio maana ya jamii forums na Great Thinkers.Ukipost kitu lazima utarajie mitazamo tofauti,sio lazima watu wakuunge mkono kwa kila wazo unalotoa hapa.

Nakuona umehama kutoka kwenye hoja ya msingi(ambayo kweli is ok) sasa unahangaika na vitu kama 'mbili' au 'zaidi ya moja' ambavyo logically is the same thing! Suppose ningesema ajira 3,5,7,10,where is the difference,huh?! Kwa nini usistick kwenye topic yako,ni ya msingi kabisa ila ina pande mbili ambazo huwezi kukwepa kuzijadili.

Binafsi mimi mwalimu wangu wa phyisics A-Level alikuwa anafundisha shule tatu na jioni anafundisha tuition.Hizi utazihesabu ajira ngapi ndugu? Tena kwa taarifa yako ajira yake ilikuwa ni katika shule ya mission na mimi nilikuwa nasoma shule ya serikali so headmaster anajua walikuwa wanaelewana vipi mpaka anakuja kufundisha shuleni kwetu.Vipi hapa je,unasemaje?

Kuna vitu unakwepa kujibu,kwa mfano,
1.ikiwa mwalimu anaweka vizuri ratiba zake,kuna madhara gani ikiwa atafundisha shule mbili au zaidi?
2.Je,ikiwa shule ina uhaba wa mwalimu wa somo fulani na headmaster akaorganize na mwl.wa somo hilo kutoka shule nyingine(kama ilivyokuwa kwetu) kuna ubaya gani?
3.Je,unafahamu kama kuna upungufu mkubwa wa walimu wa sayansi na hesabu mashuleni,wewe unashauri nini kifanyike ili watoto wetu wapate kufundishwa na walimu wachache waliopo?
4.Je,kama mbunge(mtunga sheria) anakuwa mkuu wa mkoa na mwenyekiti wa bodi ya ya pamba kwa wakati mmoja,hiyo ni sawa?
5.Je,ni ajira gani unazotaka walimu wasifanye?
6.Je,ikiwa mwalimu ana kijimradi chake nyumbani ambacho anashughulika nacho baada ya kazi,hakiitwi ajira,na je asikifanye?
8.Kwa utafiti wako umeridhika kuwa sababu kuu ya kushuka kwa elimu yetu ni utoro wa walimu,na sio kitu kingine?

Yako mengi ambayo ulitakiwa kuyafanyia kazi kabla ya kupost na kututaka tukuunge mkono hili wazo lako.
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…