Waalimu wengi wa sekondari za serikali wana ajira zaidi ya moja

Unadhani kwa mshahala wanaopata wataacha kweli kuzichangachanga mahala pengine!
 

Ndugu Mrimi,

Uko sahihi kwa kiasi fulani kwamba sikujiandaa kupokea kiasi hiki cha mashambulizi. Pengine nilijisahau kidogo kwamba nimegusa maslahi ya watu.

Napenda kusimamia hoja yangu kwa nguvu zangu zote.

Tatizo la wabunge na wenyeviti wa bodi haitoi uhalali wa kuwepo tatizo la ualimu

Upungufu wa walimu na kuwepo idadi kubwa ya walimu wahitimu wasio ajiriwa ni sehemu ya mambo yanayohitaji kufanyiwa kazi

Kuna ubaya kwa mwalimu au mtumishi mwingine yeyote wa uma kusaini mkataba zaidi ya mmoja iwapo hata mmojawapo wa mikataba hiyo hautambui uwepo wa hiyo mingine

Mwisho napenda nionyeshe furaha yangu kwamba ujumbe wangu umefika.
 
mleta maada anaonekana kuwalaumu walimu moja kwa moja, mm namshauri alaumu chanzo cha tatizo na kuanzia hapo ndo atapata mwanga wa namna ya kumaliza tatizo
 
Wewe mtoa mada ni kilaza! Hv kwan raisi ana vyeo vingapi??
Mbona madaktar pia hufanya kaz ospital zaid ya moja?
Mbona huyo mbunge yeye ni mbunge alafu n mkuu wa mkoa, watu hawasemi?? Hv una nn na sisi walimu?? Mbulula wewe we ndo unatulisha afu nina wasiwas wewe n dereva tax, hujaenda shule thats why umepost utumbo huku,afu kingne inakuhusu nn walimu kufanya kaz sehem zaid ya moja?? Kajipange uje na lingine mbuz wewe
 

Anyway,tuache habari ya wabunge kuwa wakuu wa mikoa,ni kweli wao ni haki yao kimsingi maana si watumishi wa umma,tujielekeze zaidi kwa walimu ambao ni watumishi wa umma!

Mkuu ni kweli ujumbe wako utakuwa umewafikia walengwa,ingawa hujasema walengwa ni akina nani kati ya walimu,wanafunzi au serikali.Pia ni kweli kabisa wakati wa azimio la arusha haikuruhusiwa kwa mtu mmoja kuwa na mishahara zaidi ya mmoja,ingawa hujasema kisheria kama hilo bado lipo au linafanya kazi kwa walimu tu!

Mkuu mkuu kuna kitu kingine hujaweka vizuri,hivi walimu unaosema ni wa shule za serikali tu au ni walimu wote kwa ujumla wao?
 
Nimefanya utafiti katika shule tatu za sekondari jijini Dar es salaam, na results zake nitazipublish soon. Wengi wa waajiriwa katika shule za serikali, wana ajira pia kwenye shule za private, na wengine wana ajira za part time kwenye shule mbalimbali zikiwemo za serikali na private. Katika baadhi ya maeneo shule za ziada wanaziita vidumu. Na mahali pengine wanaziita mama mdogo. Ndiyo namalizia analysis kuna mengi yamefichika katika ajira ya walimu. Baada ya kuona hawawezi kupambana na serikali kwa migomo ya wazi, sasa wamechagua njia nyingine ambayo kwa hakika mwisho wa siku anayeumia ni mtoto na si mwalimu.
Kuna uozo mwingi sana unaendelea huko mashuleni. Lakini nitaanika wote mara baada ya article yangu kuwa accepted kwenye journal. Ambapo nitachapisha matokeo hayo kwenye mojawapo ya magazeti ya kila siku, ili watanzania wajue ni aina gani ya mgomo walimu wanafanya hivi sasa.
 

Big up sana mkuu,maana wewe umeweza kutumia muda wako na kufanya utafiti.Ninachokuomba katika utafiti wako uje na data za je ni walimu wa masomo gani hasa zaidi wana ajira hizo.Na madhara(+VE na -VE) ambayo tayari yamejitokeza(sio nadharia) kutokana na walimu hao kufundisha shule zaidi ya moja.
 
Nimefanya utafiti kwa walimu wa masomo ya sayansi. Na nilikuwa naangalia ni njia zipi zinaweza kutumika kuboresha ufundishaji katika masomo ya sayansi nchini. Lakini nikaamua kuangalia kwanza mitizamo ya walimu juu ya ufundishaji wa masomo hayo ya sayansi na ni kwanini watoto hawafaulu.

Wengi wao wanaadmit moja kwa moja kwamba wapo in high demand, lakini serikali haiwajali. kwahiyo wakienda huko private schools ndiyo wanaweka energy kubwa ili waendelee kuwa na hivyo vibarua vya nje ya shule zao na wapate ujira mzuri zaidi. lakini huku serikalini ambako hawaridhiki na kipato wanalipua tu. Walimu wenyewe hawafichi hilo. wana kauli yao inaitwa "kwa maslahi ya nani"? nifanye hayo kwa maslahi ya nani? Ni mfaidishe nani?

Walimu hawana tena uchungu na ufaulu wa watoto, kwa kuwa wanasema hata wakifaulisha wanaishia kupewa shilingi 5000 kwa kila A ambayo kwao si kitu ukilinganisha na kama angepata part time job ambayo inamlipa zaidi ya mshahara wake wa serikali. Kuna mengi sana, siwezi kuyaandika yaishe hapa. Ndiyo maana nafikiri ni better kuchapisha kwenye gazeti.
 
Ina maana huku ni mwalimu na kule ni daktari?Au huku mwalimu akitoka kazini anasimamia visheti vyake?
Sijaona kama kuna tatizo lolote kwa mwalimu kuwa na ajira zaidi ya moja mradi havunji sheria.Daktari akitoka kibaruani kwenye hospitali muda wa ziada huenda kwenye dispensari kujiongezea kipato,mwalimu akipata mda wa tuition au part time ndio tatizo?
Unaonekana Researcher huna sifa ya kumiliki jina hilo kwani hulitendei haki;heading yako haiendani na content hadi ume mis-lead mjadala.Hueleweki unataka kusaidia walimu,serikali au wananchi!
Mi kama mtoto wa mwalimu nakuona kama mnafiki na usiye na nia njema na fani hii.Madaktari pale muhimbili walipo goma Serikali ilisema Itawachukua madaktari pale jeshini wawatibu wagonjwa,lakini walimu wakigoma nakuambia kambi zote zitafungwa na bado watoto wengi watabakia bila elimu.
Nakushauri usikurupuke kuja na hoja dhaifu yenye kujikamganya kwenye maswala sensitive haswa ya ELIMU.
 
me nnazo 3 ya nne nmeambiwa nifuatilie next week...ukome kutufatafata..
 

Nimefurahishwa na dhamira yako ya dhati ya kutaka kufahamu ukweli.

Labda niseme tu kwamba nimeisimamia nafasi ya mzazi na mzalendo katika kuliweka tatizo mezani. Watakaopenda kuyataja matatizo mengine hata ambayo ni sambamba na hili wanakaribishwa kufanya hivyo.Ila sifurahii sana kuona tunapinga kulizungumzia tatizo kwa kuwa yapo matatizo mengine. Pamoja na changamoto nyingine zikiwemo uhaba wa vifaa vya kufundishia kama vitabu, madarasa usafiri kwa wanafunzi, mifumo ya mitaala, mifumo ya utahini n.k. Hili la ajira zaidi ya moja naona lipo na nafurahi wachangia mada wenyewe wamelidhihirisha hilo. Nisisitize pia kwamba nnapozungumzia ajira simaanishi kumiliki biashara ndogo ndogo, kuwa na shamba au kufundisha tuisheni vipindi vya likizo. Mimi nazungumzia ajira ya kusaini mikataba, kupokea mshahara na kufanya kazi katika muda wa kazi uliotajwa katika mkataba wa kwanza kati ya mwajiri na mwajiriwa.

Kwa hiyo swali la Je wapo walimu wenye ajira zaidi ya moja? jibu lake limeshapatikana ni Ndio, ntashukuru mkikubaliana nami kwamba sikusema uongo pamoja na kutoweka ushahidi madhubuti.

Linalofuata ni kufahamu uhalali wa kisheria au kiutumishi kuhusu utaratibu huo. Na pili ni kufahamu ukubwa wa tatizo na endapo utaratibu huo ni unaathiri utoaji wa huduma za elimu au ubora wa ufundishaji. Jambo la tatu la msingi ni kufahamu chanzo cha tatizo hilo na kupendekeza namna ambalo hali hiyo inaweza kupatiwa ufumbuzi.

1. Ipo mikataba ya ajira ambayo inaweka bayana kabisa kwamba kwa kusaini mkataba huu unakiri hujaajiriwa sehemu nyingine na kwa maana hiyo hutasaini mkataba mwingine kabla ya kuuvunja mkataba huu. Hii si kwa walimu peke yao. labda mnifahamishe endapo Wizara ya walimu haizingatii kipengele hiki kwa walimu wake. hata hivyo sekta binafsi ina flexibilities katika hili, haswa pale ambapo kwa mfano shule binafsi inafahamu rasmi kwamba wanamwiba mwalimu kutoka shule nyingine. Ikumbukwe kwamba kutoa huduma za jamii kwa mfano consultancy katika fani yako inakuwa ni sehemu ya majukumu kwa baadhi ya watumishi mfano wahadhiri wa vyuo vikuu.

Je ukisaini mkataba kwa mwajiri mwingine bila mwajiri wako kufahamu ni halali kisheria?

Uduni wa mishahara na mazingira magumu ya kazi vinatajwa kuwa vyanzo vikubwa vya walimu kufikia uamuzi wa kusaini mikataba mingine. Kwa upande mwingine mwalimu anapofanikiwa kwa kufaulisha au kujenga jina hushawishiwa kufundisha sehemu zingine hata kama haikuwa dhamira yake.

Je zipo sababu zingine za walimu kufanya hivyo? Je mishahara ya walimu ikiongezwa itamaliza tatizo husika?

Ajira mbadala zinaweza kuwa ualimu au ajira tofauti, labda tu stick kwenye ualimu. Mwalimu mzoefu anaweza kusaidia kutoa huduma kwa wanafunzi wa shule zaidi ya moja. Umuhimu wa hili unajidhihirisha kwenye masomo magumu na yenye uhaba wa walimu kama hisabati. Kiuchumi si vema sana kuhodhi rasilimali muhimu kwa kumbana mwalimu mahiri katika shule moja. Hata hivyo endapo idadi ya shule anazohudumia mwalimu inakuwa kubwa, shule zenyewe zikawa mbali na ratiba kuingiliana hali hiyo inapunguza ufanisi. Hata akishawishi kwamba anajipanga sidhani kama kiwango chake kitakuwa sawa na endapo angeshika wajibu wake mkuu wa shule moja.

Kwa upande mwingine kurasimishwa kwa kwa utaratibu wa mwalimu kufundisha shule zaidi kutasaidia kuboresha idadi ya walimu na kujenga usawa miongoni mwao. Mwalimu fulani kuwepo kazini full time si tu kwa sababu hajafungua macho au somo lake si dili, au hahitaji pesa bali pengine kwa sababu hana urafiki na mkuu wa shule ampe ruhusa. Kama utaratibu wa kufundisha shule zaidi ya moja utawekwa itaeleweka bayana kwamba head cout ya walimu ni 50 lakini full time equivalence yao ni 10.

Je unadhani walimu kufundisha shule zaidi ya moja ni kutanua wigo wa utoaji wa huduma za elimu au kudhoofisha ubora wake?

Hebu tujadili hayo bila jazba kwa nia nzuri ya kuboresha elimu yetu. Nirudie tena kwamba mimi mtoa mada sijakurupuka, sina wivu na walimu natambua udogo wa mishahara ya walimu.
 
me nnazo 3 ya nne nmeambiwa nifuatilie next week...ukome kutufatafata..

Tunakuwa wepesi kuwanyooshea vidole wanasiasa na kuwaita mafisadi na wala nchi. Nakuhakikishia wala nchi ni sisi wenyewe wenye nchi!
 

Hata mtoto wa kiongozi fisadi husimama kumtetea mzazi wake huku akitambua bayana kwamba haitendei haki nchi yake. Ubinafsi ndio utakatufanya tusiutokomeze umaskini. Ungekuwa mzalendo ungepigania mzazi wako kuimarishiwa maslahi afanye kazi yake kwa uhodari na si kumuunga mkono aendelee kuwadhulumu watoto wetu akikimbiza shilingi huku na kule.
 
mi ninaposhangaaa ndio hapo ukiuliza utasikia elimu ndio ufunguo wa maisha,kwa stairi hii mtoto wa mkulima atenderea kulima na watoto wa vigogo watenderea kurisishwa madalaka na nyadhifa muhimu serikalini,eeee mungu tusaidie.
 

Narudia kuuliza tena,walimu unaowazungumzia ni walimu wa shule za serikali tu au ni walimu wote kwa ujumla???
Maana tusijekuwa tunaumiza vichwa vyetu pasipo ulazima.
 
Narudia kuuliza tena,walimu unaowazungumzia ni walimu wa shule za serikali tu au ni walimu wote kwa ujumla???
Maana tusijekuwa tunaumiza vichwa vyetu pasipo ulazima.

Nazungumzia walimu wa shule za serikali
 
mtoa maada umettumwa nini? kama we unauchungu waongeze wewe mshahara.acha kukurupuka
 

hilo lipo na linajulikana sana tu na wala siyo kwa mkuu wa shule tu bali hata viongozi wakubwa wa serikali. Issue hapa ni nani anayeumia? viongozi wetu tuliyowachagua kwa imani kubwa ya kututumikia kama walivyokuwa wakijinadi kinafiki kwenye majukwaa hawana watoto katika shule zetu hizi za st. kayumba sasa ni nani wa kumfunga mbuzi kengele?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…