kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Mpira wa miguu una wadau wengi sana duniani, Africa na Tanzania. Ukifanya kosa kwenye mpira kama mchezaji kukosa nafasi ya wazi ya kufunga, mchezaji kumuumiza mchezaji, timu kufungwa au waamuzi kuchezesha mechi vibaya Ujue unaumiza wengi sana wa jinsia, umri, dini, taaluma na hadhi tofauti kwa viwango tofauti. Wako watakaokisa furaha TU lakini wako watakaotoa machozi, kupata Sonoma, shinikizo la damu, kufukuzwa kazi na hata kujiua.
Watu wanaoumizwa na matokeo ya mpira viwanjani ni pamoja na wamiliki wa timu, viongozi wa timu, makocha, wadhamini, wanachama na mashabiki na makampuni ya kubahatisha (betting).
Mwamuzi anapokosea kwenye maamuzi yake inaweza kusababishwa na mambo yafuatayo:
1. Ubinadamu TU, bahati mbaya.
2. Mapemzi yake binafsi kwenye timu fulani kuisaidia isifungwe, isipitwe, isishuke daraja, au isikutwe kwa points.
3. Kuhongwa na wenye timu, wadhamini, mashabiki, waliobet au kampuni ya kubet.
Ili kutatua shida ya uwamuzi mbaya viwanjani lazima kufanyike yafuatayo:
1. Kuzuia makosa yasifanyike kwa kutumia waamuzi wenye taaluma kubwa,
2. Kuweka VAR viwanjani kama wengine
3. Timu kuwa na vyamzo vya mapato
4. Waamuzi kukamatwa na kuhojiwa ili kufahamu dhamira za waamuzi kuamua kama walivyoamua kwenye mechi husika.