Waandaaji Zanzibar International Marathon mlikwama wapi?

Waandaaji Zanzibar International Marathon mlikwama wapi?

TODAYS

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2014
Posts
14,747
Reaction score
24,250
Twende kwenye mada moja kwa moja.

Kwanza nawapongeza kwa hatua nyingine baada ya miaka zaidi ya kumi na kenda ya kupotea kwa mbio hizo na mwaka huu kuamua kuzirudisha kwa nguvu.

Unapozipa mbio jina la International ina maana unategemea kuwa tofauti na zile za kina Goba, Meru, sijui Ushoroba nk ikiwa na maana uwakilishi wa wakimbiaji na usanifu wake utakuwa wa hadhi ya juu.


IMG_20210720_144656.jpg


Kuna mtu naweza kumtaja ila inaweza isiwe na maana kama muhusika alijua au kutojua ethics za marathon!.

MLIKWAMA WAPI?
1. Mpakaa mkashindwa kuwapa muongozo jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani waliotakiwa kuongoza mbio za 21km kuongoza wakimbiaji?.

2. Wakimbiaji wanapishana na waendesha pikipiki na magari njiani?.

3. Mkimbiaji anadondoka njiani na anahudumiwa na wakimbiaji wenzake?.

4. Kwenye kumalizia mbio, hakuna usimamizi zaidi ya watu ambao hawakukimbia na waliomaliza kujazana kwenye finishing point?.

5. Watoaji wa 🏅 medal sijui mliwatoa wapi au hamkujipanga kwa style ya kutoa.

6. 🏅 medal zilitolewa hata kwa watu wa mtaani na ambao hawakukimbia hii ni kituko.

7. Utolewaji wa vifaa vya mbio, mtu yupo nyumbani anapiga simu na kutuma mtu apewe t-shirt, namba (nadhani) pasi kulipa!.

👉🏾Hayo tu, japo ni kadhaa yametunzwa!.

Kwa kuwa mlikuwa na kamati kubwa wakiwepo viongozi wa chama cha mbio cha Tanganyika huku serikali ya Mapinduzi Zanzibar ikiwashika mkono nadhani mlipaswa kutoa product ya kuigwa badala la kile tulichoshuhudia.
 
Karibu zanzibar wakibiaji wala urojo na ubuyu wasimamizi wa marathon vitambi boys.[emoji23][emoji23]


Lunatic [emoji2957][emoji2957][emoji2957]
 
Hapo mwishoni umetaja Serikali ya Mapinduzi, halafu bado unajiuliza walikwama wapi…!![emoji1614][emoji36]
 
Yakhee amiii.we njo uchukuwe tuuu fulana yakooo.haina shida wenye vyombo vya moto watakaa pembeni wenyewe wakiona watu wankimbiaaa.
 
Hapo mwishoni umetaja Serikali ya Mapinduzi, halafu bado unajiuliza walikwama wapi…!![emoji1614][emoIji36]
Ilidhamini kwa upande mwingine mkuu not otherwise.
 
Yakheee!! Nimeshinda mieee!! Lakini zawadi apewa Makameee!! Hii siyo sawa kabisaaa!! Bora hata marathoni za bara zina unafuuuu!!

Wazanzibari bhana!! 😁😁😁
 
Yakheee!! Nimeshinda mieee!! Lakini zawadi apewa Makameee!! Hii siyo sawa kabisaaa!! Bora hata marathoni za bara zina unafuuuu!!

Wazanzibari bhana!! 😁😁😁
Na kwa ulaji huu wa vyakula, sidhani kama kuna mzanzibari anaweza kuwa mkimbiaji maarufu wa kipindi kirefu akiwa anaishi pemba au unguja, ulaji ni mbovu sana!.
 
Back
Top Bottom