Kenyan
JF-Expert Member
- Jun 7, 2012
- 414
- 314
Waandamanaji Jijini Kisumu wamewaacha watu wengi vinywa wazi baada ya tukio la hapo jana ambapo walivamia hifadhi ya maiti ya Kwee iliyoko ndani ya Hospitali ya Rufaa ya Jaramogi Oginga Odinga.
Mochwari hiyo mpya ilifunguliwa rasmi na Gavana Anyang' Nyong'o tarehe 28 Machi mwaka huu na iliigharimu serikali ya kaunti ya Kisumu milioni 37(ksh) kununua.
Waandamanaji walivunja vioo na kuharibu geti huku wakiondoka na baadhi ya vifaa vinavyotumika katika uhifadhi wa maiti.
Gavana wa kaunti hiyo Prof Anyang'Nyong'o amelaani vikali kitendo hicho huku akiomba Jeshi la Polisi kufungua jalada la uchunguzi na kuwakamata washukiwa kwa haraka iwezekanavyo.