SI KWELI Waandamanaji Nigeria wapewa mchele ili wasitishe maandamano yaliyoanza Agosti 1, 2024

SI KWELI Waandamanaji Nigeria wapewa mchele ili wasitishe maandamano yaliyoanza Agosti 1, 2024

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Nimena video inasambaa mtandaoni ikionesha waandamanaji Nigeria wakisitisha maandamano yao baada ya kupewa mchele. Nadhani kwa Afrika ni Kenya pekee ndiyo vijana wake wanajielewa vizuri kuliko wengine.
1000103986.jpg


 
Tunachokijua
Agost 1, 2024, Maelfu ya watu waliandamana nchini Nigeria katika miji mikubwa ya nchi hiyo kudai "hatua za haraka" juu ya matatizo ya kiuchumi ya nchi hiyo, uhaba wa chakula na mfumuko wa bei.

Maandamano yalianza mapema Lagos, kitovu cha kibiashara cha Nigeria, licha ya hatua ya serikali kuzuia maandamano hayo.

Umati huo, wengi wao wakiwa ni vijana na wanaharakati wa haki za binadamu, waliandamana hadi katikati mwa jiji na maeneo ya biashara ya Ikeja, Ojota na Ojodu, huku wakiimba: "Tuna njaa, usituue, njaa na ugumu wa maisha, sera za kupambana na maskini. ,malizia ugumu sasa!"

Kwa mujibu wa ripoti ya DW, takriban watu 13 walipoteza maisha kwenye siku ya kwanza ya maandamano hayo huku wengine 300 wakikamatwa na polisi.

Wakati maandamano haya yakiendelea, imeanza kusambaa video ikionesha kundi kubwa la watu wakiwa wamebeba viroba vya mchele ambao kwa mujibu wa madai yaliyopo ni waandamani waliopewa chakula ili wasitishe maandamano yao. Video hizo zimehifadhiwa hapa na hapa.

Video hii imezua gumzo mtandaoni huku wengine wakisema siyo ya sasa.

Ukweli wake upoje?
JamiiCheck imefuatilia video hii na kubaini haihusiani na maandamano yanayoendelea sasa nchini humo. Utafutaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia Google Image Search umeonesha video hii ili ilichapishwa Mtandaoni mwezi Aprili, 2024 na ukurasa wa Linkedln wa Lagos Food Bank, siku waliyotoa kilo 10 za mchele wa msaada kwa familia maskini wakishirikiana na Aliko Dangote Foundation.

Aidha, katika kufanya uhakiki wa video hii, JamiiCheck imekutana na chapisho lingine la Aprili 17, 2024 linalodokeza juu ya msaada huo ambapo mwandishi anaishukuru taasisi ya Dangote kwa ukarimu waliofanya kwa wahitaji hao wanaopatikana maeneo ya Yoruba.
Back
Top Bottom