Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Bangladesh iko kwenye kipindi cha kihistoria baada ya waziri mkuu wake wa miaka 15 kukimbia nchi katikati ya hasira za Umma.
Wiki kadhaa za maandamano dhidi ya Serikali zimesababisha waziri mkuu Sheikh Hasina kujiuzulu, kukimbia nchi, na serikali ya muda inatarajiwa kuundwa.
Baada ya Bi Sheikh Hasina kujiuzulu na kukimbia nchi Jumatatu, umati mkubwa ulivamia makazi yake rasmi huko Dhaka huku kukiwa na ripoti za uporaji na machafuko katika mji mkuu.
Maandamano yalianza mapema Julai kama madai ya amani kutoka kwa wanafunzi wa vyuo vikuu ya kufutwa kwa mfumo wa kuandaa nafasi za kazi katika utumishi wa umma ambao ulikuwa umetengwa kwa jamaa za maveterani wa vita vya nchi hiyo vya uhuru kutoka Pakistan mwaka 1971. Tangu kuanza kwa maandamano hayo zaidi ya watu 300 wameuawa.