SI KWELI Waandamanaji wa Kenya walipora na kukimbia na farasi wa polisi

SI KWELI Waandamanaji wa Kenya walipora na kukimbia na farasi wa polisi

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Salaam Wakuu,

Kumekuwa na video inasambaa siku hache zilizopita zikidai kuwa Waandamanaji Kenya wameiba farasi wa polisi na kukimbia nao.

Mwandamanaji Farasi Fake.jpg

Video hiyo inamuonesha mwananchi anayedaiwa amepora farasi huyo akimuongoza farasi huyo kwa kasi na ustadi mkubwa. Nimeona sehemu inadaiwa yule si mwananchi. Tunaomba mfuatilie ili mtupe ukweli: video hizi hapa chini:



 
Tunachokijua
Mnamo Juni 21, 2024 nchi ya Kenya ilitawala kwenye vyombo vya habari baada ya Wananchi wake kujitokeza kufanya maandamani kupinga muswada wa fedha (Soma hapa). Maandamano hayo pamoja na kutikisa nchi ya Kenya lakini yaliambana na matukio na vioja vingi vilivyotokea kati ya Wananchi ya Kenya na Askari ambavyo vilibamba na kushika vicha vya habari.

Miongoni mwa taarifa iliyowashangaza na kuwachekesha watu wengi kwenye mitandao ya kijamii ni tukio lililomuonesha mtu akiwa juu ya fasari akimkimbiza. Baadhi ya mitandao ya kijamii (hapa, hapa, na hapa) Kurasa za Vyombo vya habari Afrika Mashariki (hapa, hapa na hapa) viliripoti tukio hilo kuwa ni Mwananchi wa Kenya ambaye amepora farasi huyo mikononi mwa polisi.

Upi ukweli wa tukio hili?
Ufuatiliaji wa JamiiCheck katika vyanzo mbalimbali umebaini kuwa video hiyo inayohusishwa na Mwananchi wa Kenya kupora farasi wa Mwandamanaji sio ya kweli kwa sababu zifuatazo:

1. Farasi anayehusishwa kwenye tukio hili sio wa polisi bali wa mmiliki binafsi wa farasi hao anayetumia jina la Malieng katika mtandao wa TikTok (Tazama hapa). Amekuwa anamiliki na kuchapisha video mbalimbali za watu wanaopanda farasi na kuzunguka mitaa ya miji mbalimbali.

1719132023369-png.3023764

Picha ikionesha Akaunti ya mmiliki wa farasi hao ikiwa na video mbalimbali

2. Video inayohusishwa na Mwananchi kukimbia na farasi wa polisi ipi katika mtandao wa TikTok toka Juni 9, 2024 wakati ambao maandamano hayo yakiwa bado hayajafanyika (tazama hapa).

1719133974061-png.3023791

Picha ikionesha video ya awali inayosambaa huku tarehe (iliyozungushiwa alama) ikiwa ni zaidi ya siku 10 kabla ya maandamano

3. Kuna video ya Juni 8, 2024 ikimuonesha mpanda farasi huyo akitoa maelekezo kabla ya kupanda farasi jambo linaloonesha safari yake ilipoanzia ambayo haioneshi kuhusisha uporaji wowote: Tazama picha hapa chini:

1719133756041-png.3023785

Picha: Picha ikimuonesha mpanda farasi akiwa kwenye haraati za kuelekeza kabla ya kupanda. Alama iliyozungushiwa ikionesha tarehe ya tukio


Zaidi ya hayo, Vyombo vya Habari TRT Afrika Swahili na Media Obsevour ya Kenya wametoa taarifa rasmi inayokanusha tukio hilo la Mwendesha Farasi kuhusishwa na Maandamano ya Juni 21, 2024 nchini Kenya. Taarifa hizo zinafafanua:

Video inayodai kwamba wapanda farasi wawili waliiba farasi kutoka kwa polisi wakati wa maandamano si ya hivi karibuni na haihusiani na maandamano. Video hiyo ilirekodiwa na kusambazwa mnamo Mei 2024 kwenye akaunti ya @tiktok_us chini ya jina la mtumiaji malieng0_0. Akaunti hiyo inashiriki video nyingi zinazoonyesha watu hao wakijihusisha na shughuli mbalimbali za kupanda farasi mjini.
Back
Top Bottom