Sam Gidori
Senior Member
- Sep 7, 2020
- 165
- 417
Kauli ya Trump baada ya kurejea White House
Rais wa Marekani, Donald Trump ameruhusiwa kurejea ikulu ya Marekani, White House, hapo siku ya Jumatatu baada ya kulazwa katika hospitali ya kijeshi ya Walter Reeds nje kidogo ya Washington DC, akipokea matibabu kutokana na kupatikana na maambukizi ya virusi vya corona.
Trump alionekana akivua barakoa na kupozi kwa ajili ya picha katika varanda ya White House, kisha akachapichapisha video katika mtandao wake wa kijamii wa Twitter akiwasihi wafuasi wake wasiogope Corona.
"Usiruhusu ikutawale. Usiiogope. Tunakwenda kuishinda. Labda mimi nina kinga ya asili, sijui," alisema Trump.
Viongozi wengine White House walioambukizwa Corona
Trump alionekana akiingia White House bila kuvaa barakoa. Hayo yanajiri wakati waandamizi wengine ndani ya ikulu ya White House wakiendelea kuambukizwa virusi vya corona. Katibu wa Waandishi wa Habari wa White House, Kayleigh McEnany pamoja na wasaidizi wengine wawili na waandishi watatu wa Ikulu wamepatikana na maambukizi ya virusi hivyo.
Umaarufu wa Trump unazidi kuporomoka
Utafiti wa maoni uliofanywa na Shirika la Habari la Reuters kwa kushirikiana na Ipos unaonesha kuwa umaarufu wa Trump umeporomoka kwa pointi 10 ukilinganisha na mpinzani wake, Joe Biden anayeongoza kwa asilimia 77. Asilimia 65 ya Wamarekani wanasema kuwa Trump asingepata maambukizi ya corona ikiwa angechukulia kwa umakini tahadhari ya kujikinga.
Biden: Barakoa zina maana kubwa
Biden, kwa upande wake, ameipinga kauli ya Trump aliyoitoa akiwataka Wamarekani wasiiogope Corona, akisema kuwa Trump alitakiwa kujifunza kutokana na aliyoyapitia.
"Ningependa kuamini kuwa Rais, baada ya kupitia aliyoyapitia - na ninafurahi kuwa anaendelea vizuri - angetakiwa kuwasilisha somo sahihi kwa Wamarekani: barakoa ina maana kubwa. Barakoa inaokoa maisha, inazuia maambukizi ya corona," alisema Biden.
Mdahalo wa Oktoba 15
Biden, ambaye hakupatikana na maambukizi ya virusi hivyo, amesema kuwa yupo tayari kushiriki katika mdahalo wa pili unaotarajiwa kufanyika Octoba 15. Timu ya Trump imesema kuwa mgombea wao pia yupo tayari kushiriki katika mdahalo huo.
Hata baada ya kurejea White House, Trump anatarajiwa kupata upinzani mkubwa zaidi, baada ya idadi ya vifo na maambukizi ya virusi vya corona kuonekana kuongezeka ndani ya ikulu ya Marekani, hata katika bunge la Congress, ambapo Maseneta watatu wamepatikana na maambukizi.
Kwa sasa, Trump anaendelea kupatiwa matibabu ndani ya White House kwa takriban siku 5 zijazo huku akitakiwa kuendelea kujitenga.