Pre GE2025 Waandikishaji wa Tume Huru ya Uchaguzi waapishwa ili "kutunza siri" za ukumbi wa Halmashauri. Ni siri gani wanazopaswa kutunza?

Pre GE2025 Waandikishaji wa Tume Huru ya Uchaguzi waapishwa ili "kutunza siri" za ukumbi wa Halmashauri. Ni siri gani wanazopaswa kutunza?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Wakuu,

Naona zoezi la uandikishaji linazidi kuwa la moto, naona waandikishaji sasa hivi washaanza kula viapo huko

Kwenye taarifa ya tume hawa waandikishaji wameapa "kutunza" siri za Ukumbi wa Halmashauri.

Sasa najiuliza hizi siri wanazotakiwa kutunza ni zipi ambazo wananchi hawatakiwi kujuq? Uchaguzi ni jambo linalotakiwa kuwa wazi, kama ni hivyo hawa waandikishaji wanatunza siri gani ambazo wananchi hatutakiwi kujua?

Au wanamaanisha taarifa za watu wanaojiandikisha?

Nadhani kuna haja ya Tume kutolea ufafanuzi wa hizo siri ambazo hawa watu wanatakiwa kutunza!

================================================

Hakimu Mwandamizi wa Mahakama ya Mwanzo Kigamboni Ndg.Joyce Akyoo akiwaapisha watendaji ngazi ya Jimbo kiapo cha kujitoa uanachama wa chama cha siasa na kile cha kutunza siri katika ukumbi wa Halmashauri Manispaa ya Kigamboni leo tarehe 10 Machi, 2025.

Mafunzo ya watendaji wa uboreshaji yameanza leo katika Halmashauri hiyo pamoja na Halmashauri zote za mkoa wa Dar es Salaam.

Snapinst.app_482317033_1818551802278061_855735558229461758_n_1080.jpg


Snapinst.app_483167380_1818551875611387_5004542483235717937_n_1080.jpg


Snapinst.app_483480325_1818551922278049_4573767188315710980_n_1080.jpg
 
Back
Top Bottom