Waandishi wa Habari na Bahasha: Sio Kila Bahasha ni Rushwa

Nakumbuka waandishi wawili waliniandika vibaya baada ya bahasha kuisha...huku wengine wakitoa habari nzuri baada ya kuwapa bahasha

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Wanako fanya kazi hawalipwi? Kwa hiyo hata hakimu,mwalimu, injinia, polisi, mwanajeshi, daktari n.k ili afanye kazi lazima apewe bahasha tutafika?
 
Waandishi wa habari wa Tanzania mnatia aibu sana kwa kuendekeza njaa kupita kiasi!

Juzi kati nilihudhuria mkutano wa siasa uliokuwa ukiendeshwa na chama kimoja cha siasa. Baada ya kuisha kwa mkutano, nilishuhudia kundi la waandishi wa habari, hasa wa kike, wakimzingira kada wa chama aliyekuwa akiendesha mkutano ule. Nikadhani labda wanaenda kumhoji ili kupata habari zaidi.

Lakini niliposogelea karibu nilishangaa kuona wale akina dada wanamuomba fedha huku wengine wakijipendekeza kwa kumpongeza kwa hotuba nzuri. Kada aliwagawia noti chache alizokuwa nazo na wale waliokuwa hawajapata mgawo wa noti waliambulia sarafu chache alizokuwa nazo mfukoni.

Ndugu zangu, waandishi wa habari mnatia aibu sana. Hivi huwa hamlipwi mishahara na waajiri wenu? Sasa kwanini mnajirahisisha hivi kwa makada wa vyama kama kunguru wenye njaa? Sio pouwa hivyo mnavyofanya ndugu zangu.

Ni muda mrefu sasa mmekuwa na tabia hii ya ufisi. Acheni kuwa tegemezi na kujikomba kwa makada wa vyama kugombea chenji za kipuuzi!


:yield:
 

Dawa ya njaa ni shibe!.
[h=3]Waandishi wa Habari na Bahasha: Sio Kila Bahasha ni Rushwa!, nyingine ni "mshiko tuu!"..[/h]
Pasco
 
Mkuu tpaul ni afadhali umekuja kuongea. Ila inakera inasikitisha na pia nahisi wenyewe wanafurahia tu na hawako tayari kufanya mabadiliko. Nadhani liko tatizo kubwa kuliko vile tunavyodhani lakini je nani atasaidia kama si wao wenyewe Na tena hao wanawake ndio wa kuwahurumia kabisaaa maana watoa habari (sources) wakiwaona basi ni tabu. Utawaonea huruma ni kama kondoo anajipeleka kwa chatu amezwe.
Wanafikia hatua ya kugombana kwa ajili ya hawa sources of information kwa kuwa wanakua more than sources of information wanakua "sources" sijui unanielewa I mean "sources" Unapigana na mwanahabari mwenzio kwa sababu ya a married guy you claim to have working relationship, that's insane. Liko tatizo beyond the way we think!
 
Wanako fanya kazi hawalipwi? Kwa hiyo hata hakimu,mwalimu, injinia, polisi, mwanajeshi, daktari n.k ili afanye kazi lazima apewe bahasha tutafika?

Umeona enh...?Pasco wacha kuleta tafsiri nzuri nzuri huu ni "MLUNGULA" uite majina yote unayoweza lkn mnaharibu taalumu hii adhimu kwa kupenda kwenu "vi-bahasha vya khaki"!
 
Wengine hasa wanawake huwekewa bussiness card za viongozi mnnimeona hii live nikiwa shirika moja tuliwafungia alfu hamsini waandishi 15 kilammoja kabla ya kuwagaia bosimmoja aakatuita akawa anatoa dir Yule muweke bcard Yule usiweke

Nilishhtuka mpakaleo hii zilepesa sijui ziliaandikwa za nini na auditor alipokuja akatoa chetisfikabisa alha
 
Sasa hiyo ya bussiness card wenyewe wakizikuta wanashukuru Mungu na anapiga simu fasta wakutane Tamal hotel usiku, inatia huruma hawajatambua thamani ya utu wao kwa kweli hii ni zaidi ya njaa.
 
Sasa hiyo ya bussiness card wenyewe wakizikuta wanashukuru Mungu na anapiga simu fasta wakutane Tamal hotel usiku, inatia huruma hawajatambua thamani ya utu wao kwa kweli hii ni zaidi ya njaa.

Ni kweli mkuu ila tuwaombee sio wao roho ama Pepo la Shortcut ....
 
Nimelikumbuka bandiko hili kufuatia kushutumiwa mahali eti naandika baada a kuvuta kitu mahali!.

Paskali
 
Nimelikumbuka bandiko hili kufuatia kushutumiwa mahali eti naandika baada a kuvuta kitu mahali!.

Paskali
Pascal, jifunze..sio lazima uzungumze kila kitu. Sio lazima kila jambo ulisemee!

Unaweza kunyamaza na mambo yakaenda tu! Ukitaka kulisemea kila jambo kuna muda utakuwa unajikanyaga tu!
 
Pascal, jifunze..sio lazima uzungumze kila kitu. Sio lazima kila jambo ulisemee!

Unaweza kunyamaza na mambo yakaenda tu! Ukitaka kulisemea kila jambo kuna muda utakuwa unajikanyaga tu!
Asante kwa ushauri.
Paskali
 
Pascal Mayalla. Naomba utuwekee CV yako binafsi Nina mashaka na wewe
Au unataka Vyeti?.

Paskali
 
Kaka wengi humu hawajielewi na hawafahamu status za watu wanadhani wote ni watu wakupelekwapelekwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…