Waandishi wa Habari na Bahasha: Sio Kila Bahasha ni Rushwa

Au unataka Vyeti?.

Paskali
 
Wanabodi, japo tukio hili waandishi tumedhalilishwa, haya ndio mambo niliyoyasema kwenye bandiko hili,
Kufuatia bahasha za khaki kuwa ni haki na stahiki za waandishi, sasa tumefikia kudhalilishwa kwa kutupiwa kama mbwa!.

Sasa every Tom, Dick and Harry anaweza kuwa mwandishi, matokeo yake, makanjanja ambao hawakupita shule yoyote ya habari, hawajui maadili, wanatupiwa pesa kama mbwa na kuanza kugombania, hivyo kutuaibisha waandishi wote tuonekane ni watu wa hovyo, hatuna maana!..
P.
 
Leo kwenya kipindi cha Jicho Letu Ndani ya Habari, kinachorushwa mubashara na Star TV kila Jumamosi asubuhi, leo kukaibuka hoja ya waandishi kupokea bahasha, ambayo iliibua mjadala mkali kwa Aloys Nyanda kuwalipua waandishi wa Mwanza akiwamo Mansur kushikishwa kidogo dogo na Mniwasa hivyo waandishi wakaishia kuifagilia tuu badala ya kuandika shida za maji za wananchi, Nyanda akasema this is not right.

Mansour akijibu tuhuma amekiri waandishi kupokea bahasha nene na kusema hizi ni bahasha halali za posho kama posho nyingine zozote halali ambazo sio rushwa. Mansour naye akamlipua Nyanda kupokea posho nene kumsafisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda aliposusiwa na media baada ya uvamizi wa Clouds, Nyanda alilipiwa tiketi ya ndege na posho nene ya kujituma kwa kumtoa Mwanza hadi Dar kulikofanyika mahojiano hayo, hali iliyopelekea badala ya Nyanda kumuuliza Makonda maswali magumu, aliishia kumbeba!.

Naendelea kusisitiza, kuna aina mbili za bahasha kwa waandishi, bahasha genuine za empowerment kama logistics support, kama usafiri, lunch, overhead costs na posho za kujikimu kuwawezesha waandishi kutimiza majukumu yao kikamilifu ambapo hadi Ikulu wanafanya, na kuna bahasha haramu za rushwa ku influence positive coverage or ku suppress habari fulani isitoke.

Tatizo ni the dividing lines between bahasha hizo mbili is very thin.

P.
 
Kweli kabisa. Waandishi wa habari 'njaa' ndio pia wanashindwa kuandika maovu yanayofanywa na serikali ya awamu ya tano na badala yake kuishia kusifia tu. Hili suala linachangia sana kudidimiza uandishi makini na kukuza uandishi wa kikanjanja.
 
Wanabodi,
Leo ni siku ya kimataifa ya uhuru wa habari, kila mwaka sisi waandishi huwa tunakutana mahali kwa siku 2 na kujadili mambo mbalimbali kuhusu uhuru wa habari, na katika mkusanyiko huo, serikali, vyama vya habari na Taasisi za habari hutoa matamko kede kede kuhusu uhuru wa habari, lakini kwa mwaka huu, kufuatia janga la Corona, hakuna maadhimisho yoyote rasmi ya kukutana, ila nilitegemea wizara ya habari, vyama vya habari na mashirika na Taasisi za habari zitoe matamko mbalimbali.

Bado sijabahatika kuona tamko lolote!, ila usikute zile speech huwa zinaandaliwa kwa ajili ya presentations kwenye kongamano hotelini, safari na per diem!, leo hakuna safari, no trip, no per diem, no hotel gathering, hivyo this time hata speech tuu hakuna?!.

Nawatakia waandishi wenzangu, maadhimisho haya ya kimya kimya, nawashauri wale wafadhili mbalimbali wa tukio hili, kwa vile hatukusafiri, wala kula na kulala hotelini, then naomba hao wafadhili watutumie tuu hizo per diem, tutahama majumbani mwetu na kuhamia hotelini 3 days kisha tutatoa matamko.

Paskali
 
One, hakuna critical thinkers, sioni hata kidogo, Mtu kama wewe uko media unaweza ukawa vilevile ni informer, I had witnessed you guys when you scramble for those envelops full of money.
Mkuu Interested Observer , kwenye hili la critical thinkers wapo ila wameamua ama kukaa kimya ama they don't think critically anymore, instead they think positive kuisaidia nchi kupata maendeleo kwa powers of positive thinking.

Hili la media ku scramble for those little brown envelopes ni kweli lipo na linatudhalilisha, ila sio waandishi wote tuko hivyo, mimi being one of them ambao hatupokei bahasha na tunalaani udhalilishaji huo wa kuwapa bahasha waandishi kwa mtindo huo wa kudhalilisha.

Media, Tumedhalilishwa!, Tumejidhalilisha!. Ni Matokeo ya Sheria Mbovu, Umasikini, Dawa ni Kuunganisha Habari na UtangazajI, Tulipwe Fungu Nene!.

Sio kila bahasha ni rushwa, nyingine ni sitting, nyingine ni logical support
Waandishi wa Habari na Bahasha: Sio Kila Bahasha ni Rushwa - Pasco wa JF!
P
 
Nawatakia waandishi wenzangu wote wa habari, maandimisho mema ya siku hii ya kimataifa ya uhuru wa habari.
P.
 
Mkuu paskali.
Nashukuru kwa andiko lako linalochochea tafakuri.

Ama nikuulize ana ya uandishi uliouweka hapa, kuna gaps yaani spaces kubwa kutoka theme moja kwenda nyingine.

Unaweza kurekebisha kuondoa hizo gaps ili kutiririsha mada vyema?
Naisoma upya thread
 
Tanzania waandishi wa habari tupo sana na hizo bahasha tunazipokea sana tuu kama wazazi wanapo pokea posa!. Waandishi wa Habari na Bahasha: Sio Kila Bahasha ni Rushwa
P
Nikiwa bado nasoma nilikuwa naongea na muandishi mmoja (RIP)anaitwa Nzo, nilimuambia nataka nisome niwe muandishi wa habari kama yeye, cha kushangaza hakunijibu, nikamsemesha tena kwa mara ya pili pia hakunijibu akatazama pembeni.
Kwa miaka zaidi ya 20 nilijiuliza sana kwanini Nzo hakutaka kunishauri kuhusu kufanya fani ya uandishi wa habari ila miaka ya hivi karibuni ndiyo nimejua kuwa hiyo fani ni mayala kali sana hailipi bila bahasha za kaki ambazo ni wazi husababisha waandishi kufikiri kwa kutumia tumbo.
Nashukuru sikuingia kwenye hiyo fani aisee.
 
Poti hapa siyo ni mlungula.
 
MEI 3 ya kila mwaka ni Siku ya Kimataifa ya Uhuru wa vyombo vya habari, Mimi Pascal Mayalla, kwa niaba yangu kama mwanahabari ambaye ni mwandishi wa habari huru na wa kujitegemea kwa kujitolea na kwa niaba ya kampuni yangu ya PPR as chombo huru cha habari, niwatakie wanahabari wenzangu wote, maadhimisho mema ya siku hii, huku nikidurusu, niliwahi kusema nini kuhusu uhuru wa habari kwa media zetu za Tanzania yetu.

Nawatakia maadhimisho mema ya siku yetu hii ya leo na uhuru wa habari mwema.
Paskali.
 
Hatuwezi jua labda kuna bahasha kaki kasogezewa maana anatumia gharama kubwa sana kuandika nakala zake didhani kama anatoa hela yake mfukoni
Mkuu wa stendi , news ni bure, kuandika ni bure, situmii gharama yoyote apart from time, mimi ni mwandishi wa habari wa kujitegemea kwa kujitolea, naandika bure kwa kujitolea silipwi na yeyote!.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…