Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Katika hali isiyotarajiwa waandishi wa habari na wadau wengine wanaotajwa kutohusika moja kwa moja na uchaguzi, wameondoshwa kwenye ukumbi wa uchaguzi wa Baraza la Vijana la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAVICHA) Taifa kutokana na kile kilichoelezwa kuwa kwa sasa wanaostahili kubali ni wale tu waliotajwa kuwa ni wahusika wa moja kwa moja na uchaguzi huo
Maamuzi hayo yametangazwa na Msimamizi wa uchaguzi huo Salum Mwalimu mbele ya wajumbe wa mkutano mkuu wa BAVICHA Taifa unaoendelea sasa (leo, Jumatatu Januari 13.2024) kwenye ukumbi wa Ubungo Plaza, jijini Dar es Salaam
Salum Mwalimu ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Zanzibar amesema kuwa kwa sasa wanaohitajika kubaki ukumbini hapo ni wagombea, wapiga kura ambao ni wajumbe wa mkutano mkuu wa BAVICHA Taifa, wasimamizi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi huo wakiongozwa na Prof. Azaveli Lwaitama, maafisa wa chama wanaofanya kazi maalum kama vile kuchapisha nakala mbalimbali, pamoja na wale wanaohusika na ulinzi ambao nao pia amesema itafika wakati wataondolewa.
Soma Pia: Japo baadhi wanampinga sana tajiri Mbowe, Wajumbe wa Baraza Kuu BAVICHA walia kutolipwa posho zao
Amesema Waandishi wa habari wataruhusiwa kurudi ukumbini hapo wakati wa kutangazwa kwa matokeo ya jumla, lakini kwa sasa shughuli zote zinazoendelea ukumbini hapo kama vile kujinadi kwa wagombea, upigaji wa kura na uhesabuji wa kura hazitaonekana na wanahabari, ingawa amebainisha kuwa zoezi la upigaji na uhesabuji wa kura litakuwa la wazi na kufanyika huku wajumbe wote wa mkutano mkuu wakishuhudia
"Waandishi wa habari mtupishe tutawaita wakati wa kutangaza matokeo, sasa hivi humu ndani wabakie wagombea, wapiga kura, wasimamizi wa uchaguzi na walinzi na hata wenyewe pia baadaye nitawatoa tubaki sisi tu" -Mwalimu
Awali mkutano huo ulianza kwa kufunguliwa na Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman Mbowe, ambapo pia ilishuhudiwa viongozi mbalimbali waalikwa kutoka ndani na nje ya chama hicho wakitoa salamu zao kwa wajumbe wa mkutano, ambapo imeshuhudiwa Tundu Lissu, John Heche, Odero Charles Odero, Abdul Nondo na wengineo wakitoa salamu, huku Mwenyekiti wa BAVICHA Taifa anayemaliza muda wake John Pambalu naye akishuhudiwa akitoa hotuba ya kuaga...